July 23, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuwasili salama, kikosi cha Simba kimeanza rasmi mazoezi katika jiji la Instabul nchini Uturuki kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Simba wamewasili jana jijini humo wakiwa na Kocha wake mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems aliyerithi mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye alimaliza mkataba wake.

Kikosi hicho kitakuwa jijini humo kwa wiki mbili na kikitarajia kucheza mchezi takribani tatu au mbili za kujipima na klabu kadhaa nchi hiyo ili kujiweka fiti kabla ya kurejea Tanzania.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Simba, Haji Manara, amesema dhumuni na malengo ya kukipelekea kikosi Uturuki ni kuwapa wachezaji utulivu na kuelewana mapema kutokana na baadhi kuwa wageni kabla ya ligi kuu msimu wa 2018/19 kuanza.

Katika ratiba mpya ya ligi msimu ujao inaonesha Simba wataanza kibarua chao dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons Agosti 22 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

1 COMMENTS:

  1. Safisana simba na uongozi kwa ujumla maana simba ya sasa nisimba moto inafrahisha kwakweri
    One love simba nguvu moja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic