July 12, 2018


Na George Mganga

Wakati ukiwa umesalia mwezi mmoja pekee kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Bodi ya Ligi kupitia kwa Mkurungezi wake Boniface Wambura, imesema tayari imeshakamilisha kupanga ratiba.

Wambura ameeleza kuwa ratiba tayari imeshawasilishwa katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kufanyiwa mapitio ambao kitachakosubiriwa ni mrejesho kama kuna marekebisho ifanyiwe kabla ya kutolewa hadharani.

Mkurugenzi huyo amesema ratiba imezingatia kila kitu ikiwemo mashindano ya CAF ambayo mwaka huu yatakuwa yanaanza mwishoni mwezi Disemba hivyo wameipanga kulingana na uwepo wake.

Uwepo wa mashindano ya CAF, FIFA pamoja na mengine ndani ya nchi yamewafanya Bodi ya Ligi kuipanga ratiba vema ili baadaye kusije kukawa na upanguaji tena kama ambavyo imekuwa ikifanyika mara kwa mara pindi ligi inapoanza.

"Ratiba tayari tumeshaiandaa na imeshafika kwenye ofisi za TFF, tunachokisubiri hivi sasa ni mapitio ili kama kuna marekebisho tutaifanyia. Tumezingatia uwepo wa mashindano ya CAF pamoja na FIFA pia ya hapa nchini ili kutoleta mkanganyiko" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic