July 12, 2018


Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga wameibuka kuzidi kutoa madukuduku yao kuhusiana na suala la Abbas Tarimba kuizulu kwenye Kamati ya Kuivusha Yanga wakati wa mpito.

Wanachama hao kutoka tawi la Tandale kwa Mtogole wameeleza kuwa kaimu Mwenyekiti wao, Clement Sanga amekuwa anaiendesha klabu kwa namna anavyotaka kuliko kuonesha kama yeye ni mtu wa mpira.

Mmoja wa wanachama kutoka tawi hilo amesema kuondoka kwa Tarimba ni kama pigo kwa Yanga kutokana na uweledi wake katika kazi kitu ambacho kimesababisha kila mtu kuibuka na maoni yake tofauti juu ya Sanga.

Aidha ameeleza kitendo cha kuivunja kamati kimyakimya si busara bila kukutana na Tarimba mwenyewe ambaye ni ndiye Mwenyekiti Mkuu.

Ikumbukwe Tarimba alipitishwa kushika wadhifa huo kupitia Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika Juni 10 2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam lakini hajamaliza hata miezi mwili ametangaza kujiuzulu.

Tarimba anakumbukwa na wanayanga kwa kuanzisha suala la Yanga kuwa kampuni kipindi akiwa kiongozi ndani ya klabu hiyo wakati huo kukiwa na kundi la Yanga asili waliokuwa wakipinga mchakato huo kutoka kwa Tarimba.


2 COMMENTS:

  1. Cha msingi ni kuungana na kujenga timu has a katika hiki kipindi kigumu cha financial crisis. Acheni kutumiwa na viongozi mtauwa Tim

    ReplyDelete
  2. HUYO SANGA MSENGE SANA MAMAE ZAKE....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic