Siku chache baada ya kuanguka saini katika kikosi cha Simba, Hassan Dilunga tayari amejiunga na kikosi cha Simba nchini Uturuki.
Dilunga ametokea Mtibwa Sugar lakini aliwahi kuichezea Yanga ambayo baada ya kung'ara kwa msimu mmoja, baadaye iliamua kuachana naye.
Simba imeweka kambi katika milima ya Kartepe nchini Uturuki kujiandaa na msimu ujao wa 2018/19.
Dilunga ametua Uturuki akiongozana na Said Ndemla, Erasto Nyoni pamoja na Meddie Kagere.
Hali ya hewa ya ukungu imetanda katika enero la milima ya Kartepe nchini Uturuki, lakini chini ya Kocha Patrick Aussems raia wa Ubelgiji, Simba imeendelea kujifua.








Hongera Simba kwa kuondosha utata juu ya usajili wa Dilunga kwani watu hasa wa upande wa pili ulishaanza kuzalisha fitna mitaani juu ya usajili wake.
ReplyDelete