July 16, 2018


Kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga, ameibuka na kukanusha taarifa zilizoripotiwa kupitia mitandao na vyombo vya habari kuwa amejiunga na klabu ya Simba.

Picha za kiungo huyo zilisambaa kwa kasi juzi zikionesha anasanini mktaba mpya na wekundu hao wa Msimbazi ambao ulioelezwa kuwa ni wa miaka miwili.

Kupitia Radio One, Dilunga amekanusha na kusema alipewa kuangalia mkataba pekee lakini hakuweza kusaini huku akieleza bado wapo kwenye mazungumzo na Simba.

"Hapana sijaini, nilikabidhiwa tu mkataba ili niuangalie, bado tupo kwenye mazungumzo na kama tukifia mwafaka nitawaeleza" alisema.

Wakati Saleh Jembe ikiwa ni moja ya blog zilizoripoti taarifa za Dilunga kusaini Simba, uhakika wa taarifa kutoka Simba zinasema tayari ameshamalizana na mabosi hao ambao hivi sasa wana jeuri ya fedha za Mohammed Dewji.

Simba inaingia kambini hapo kesho tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

2 COMMENTS:

  1. Vijana siku hizi .... wanapishana na ukweli. Mbona picha inaonyesha kasaini na anaweka dole gumba sasa habari ya kusema alipewa tu mkataba kuuangalia anazingua?

    ReplyDelete
  2. unaweza kuta ni picha ya mwaka jana..alafu vyombo vya habari vinaitumia. Mbona hata huyu mwandishi mwenyewe hasemi kama picha hii walimpiga siku hiyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic