July 7, 2018


Timu ya taifa ya England imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia Urusi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sweden.

Mabao ya England yamefungwa na Harry Maguire (30') pamoja na Dele Alli aliyefunga katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili.

Ushindi huo unawafanya England kuingia hatua hiyo ya nusu ikiwa ni baada ya miaka 24 ambapo mara ya mwisho ilikuwa 1990.

Baadaye majira ya saa 3 kamili usiku, Croatia watakuwa kibaruani kukipiga dhidi ya wenyeji Urusi.

Kumbuka tu kuwa mechi zote hizi zinaonekana mbashara kupitia king'amuzi cha Star Times.


1 COMMENTS:

  1. Kwa haraka sijamuona mchezaji wa kikosi cha timu ya Uingereza anaecheza soka nje ya England. Hapa kuna funzo kubwa kwa wadau wenye fikra potofu na ya uoga yakwamba kuruhusu wachezaji wengi katika ligi kama hii ya ya kwetu hapa Tanzania itakandamiza viwango vya wachezaji wazawa. Uingereza ilikuwa na kasumba kama ya hii hapa mwanzo na kuziachia nchi kama Italy zikinufaika na uwepo wa wachezaji wa kigeni waliokuwa wakiwapa wachezaji wao changamoto za kutosha. Hakuna kinachoibeba Uingereza hivi sasa katika timu yao ya taifa isipokuwa ni uwepo wa rundo la wachezaji wa kigeni wanaowapa wachezaji wao wazawa changamoto tosha zilizopelekea kuinua viwango vya wachezaji wao wanaotesa kule Urusi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic