July 13, 2018



 YANGA, jana iliwatambulisha nyota wawili wapya, Feisal Salum Ab­dallah ‘Fei Toto’ kutoka JKU ya Zanzibar iliyo­mpa mkataba wa miaka mitatu na Jaffar Moham­med aliyekuwa Majimaji aliyepewa mkataba wa miaka miwili.


Katika usajili huo, gumzo kubwa lilikuwa ni usajili wa Fei Toto ambaye kabla ya jana jioni Yanga haijamtan­gaza kuwa mchezaji wao, asubuhi yake, Singida United ilimtambulisha imemsa­jili kwa kumpa mkataba wa miaka mitatu.


Usajili huo ilikuwa kama filamu kwani asubuhi Mku­rugenzi wa Singida United, Festo Sanga, alitangaza wamemsajili mchezaji huyo na kusambaza picha pamoja na video zinazoonyesha uthibitisho wa hicho kilicho­fanyika.

Haikupita muda mrefu, jioni Yanga ikamtambuli­sha Fei Toto klabuni kwao ambapo katika utambulisho huo, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika ndiyo walihusika.

Mbali na Singida kutan­gaza kumsajili Fei Toto kabla ya Yanga haijapindua meza kibabe, Simba nayo inatajwa ilikuwa ikimuhitaji mchezaji huyo na ilibakia kidogo wampe mkataba, ikashindikana.

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa mara baada ya kukamilisha usajili huo, Nyika alisema: “Ndiyo tumeanza kazi katika usajili wetu, tu­lianza na Mohammed Banka, leo (jana) tumemalizana na wachezaji hawa wawili.
 
“Usajili huu tunaufanya kwa weledi mkubwa tuki­fuata matakwa ya mwalimu wetu Mwinyi Zahera kwani aliagiza anataka tuimarishe kwenye nafasi ya kiungo na hata ukiangalia, Fei Toto, Jaf­far na Banka, wote wanach­eza nafasi hizo.”

Naye Meneja wa JKU ambaye pia ni meneja wa Fei Toto, Mohammed Kombo ‘Afande Chimoudy’, alimaliza utata kwa kusema: “Kuanzia leo (jana Alhamisi), Feisal ni mchezaji rasmi wa Yanga baada ya kumalizana nao kwa kila kitu.

“Licha ya Singida kutangaza wamemsajili, lakini hawezi kuwa mchezaji wao kwa sababu walishindwa kufuata utaratibu, wao waliongea na mchezaji mwenyewe wakashindwa kutufuata sisi viongozi. Jambo kama hili lililofanywa na Singida ha­likubaliki na ingekuwa kuna uwezekano timu kama hizi zikafungiwa.”

Kwa upande wa Fei Toto, alisema: “Kuanzia sasa mimi ni mchezaji wa Yanga na naahidi nitafanya makubwa ndani ya timu hii. Ni kweli Singida na Simba walinifuata lakini nimeamua kuja Yanga kwa sababu nimeona ndiyo sehemu sahihi kwangu.”

Wakati hayo yakijiri, taarifa kutoka Simba zinasema kuwa, walikuwa wamekaribia kumsajili Fei Toto ambapo walimtengea kitita cha Sh milioni 30 na mshahara wa Sh milioni mbili pamoja na gari, lakini mchezaji huyo alishindwa kusaini Simba baada ya vigogo wa Yanga kumficha nyota huyo.

Singida waja juu
Baada ya utambulisho huo wa Yanga, Mkuru­genzi wa Singida United alitoa tamko kwa kusema: “Feisal tumemsaini kwa mkataba wa miaka mitatu tukiwa tumekutana naye chini ya mwanasheria na wakala wake na mchezaji mwenyewe alikubali kusaini na sehemu kubwa ya fedha ameshachukua.

“Hajasaini ‘pre contract’ kama watu wanavyosema, ile ni ‘contract’ inayotam­bulika na ndiyo itatumika kwenye usajili wake kama ambapo tutakuwa tumefi­kia makubaliano ya kumsa­jili pale TFF watakapoamua.

“Sisi tunajua mche­zaji huyu amesajili Singida United, haya ambayo yametokea kwamba amesajili Yanga ni ‘double standards’ kwa sababu linawaweka Watanzania njia panda. Sisi tunaamini vyombo vinavyohusika na usajili ambavyo ni Bodi ya Ligi na TFF vitaamua jambo hili kwani tumeshamalizana na JKU.”

CHANZO: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. HUO USHAURI KAMA NI WA KOCHA BASI ANAWADANGANYA, SHIDA YA YANGA NI NAFASI ZIFUATAZO NAMBA 5, 6, 7, 9, 11, MNATAKIWA MSAJILI BEKI WAWILI WA KUTOKA NJE, NA KIUNGO MKABAJI SIO WAKINA MAKAPU NA ANDREW VINCENT WANAOKABIA MACHO!!!

    ReplyDelete
  2. SHIDA YA YANGA NI NAFASI ZIFUATAZO NAMBA 5, 6, 7, 9, 11, MNATAKIWA MSAJILI BEKI WAWILI WA KUTOKA NJE, NA KIUNGO MKABAJI SIO WAKINA MAKAPU NA ANDREW VINCENT WANAOKABIA MACHO!!! MBONA MNATAFUTA WA BEI CHEE!!!...TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WA MAANA KWA NAFASI ZA NAMBA 5, 6, 9, 7 NA 11.......NAANZA KUMWAMINI TARIMBA KUWA UONGOZI WA YANGA NI WA UBABAISHAJI NA WASANII TU, KUWADANGANYA WAPENZI WAO.....NA KAMA UONGOZI HUU UTAENDELEA NA MTINDO HUU....UBINGWA UTAKUWA WA SIMBA, AU AZAM.....SIDHANI KAMA WACHEZAJI DIZAINI HIZI WANAWEZA WAKASHINDANA NA TIMU KAMA SIMBA AU AZAM ZENYE VIKOSI KIPANA AMBAPO UNAWEZA UKAPATA HADI VIKOSI 2......TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WENYE UWEZO WA HALI YA JUU WATAKAOLETA USHINDANI....
    HUYO KOCHA ANAWALOSTISHA NA KUWASHAURI VIBAYA!! KAMA MNATEGEMEA KUSHINDANA NA KUTWAA UBINGWA KWA WACHEZAJI DIZAINI HIZI!!!!...YANGA INAKUWA KAMA LIPULI AU PRISON KWA USAJILI WA WACHEZAJI KAMA HAWA!

    ReplyDelete
  3. SHIDA YA YANGA NI NAFASI ZIFUATAZO NAMBA 5, 6, 7, 9, 11, MNATAKIWA MSAJILI BEKI WAWILI WA KUTOKA NJE, NA KIUNGO MKABAJI SIO WAKINA MAKAPU NA ANDREW VINCENT WANAOKABIA MACHO!!! MBONA MNATAFUTA WA BEI CHEE!!!...TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WA MAANA KWA NAFASI ZA NAMBA 5, 6, 9, 7 NA 11.......NAANZA KUMWAMINI TARIMBA KUWA UONGOZI WA YANGA NI WA UBABAISHAJI NA WASANII TU, KUWADANGANYA WAPENZI WAO.....NA KAMA UONGOZI HUU UTAENDELEA NA MTINDO HUU....UBINGWA UTAKUWA WA SIMBA, AU AZAM.....SIDHANI KAMA WACHEZAJI DIZAINI HIZI WANAWEZA WAKASHINDANA NA TIMU KAMA SIMBA AU AZAM ZENYE VIKOSI KIPANA AMBAPO UNAWEZA UKAPATA HADI VIKOSI 2......TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WENYE UWEZO WA HALI YA JUU WATAKAOLETA USHINDANI....
    HUYO KOCHA ANAWALOSTISHA NA KUWASHAURI VIBAYA!! KAMA MNATEGEMEA KUSHINDANA NA KUTWAA UBINGWA KWA WACHEZAJI DIZAINI HIZI!!!!...YANGA INAKUWA KAMA LIPULI AU PRISON KWA USAJILI WA WACHEZAJI KAMA HAWA!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic