GOR MAHIA WATAJA DAWA ITAKAYOWAMALIZA YANGA JULAI 18 KENYA
Baada ya kuondoka nchini jana kurejea kwao Kenya, uongozi wa Gor Mahia umefunguka kuhusiana na dawa waliyoiandaa ili kuimaliza Yanga Julai 18 2018.
Gor Mahia itakuwa inaanza maandalizi yake kesho Jumatatu huko Nairobi kwa ajili ya kubaliana na Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya michuano ya KAGAME kumalizika.
Kwa mujibu wa Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr, amesema kikosi chao hakikuja na mziki wote wa wachezaji akieleza kuna baadhi ya nyota ambao hajawaweka wazi watakipiga na Yanga.
Kerr amesema aliamua kufanya hivyo akiwa kama Kocha Mkuu ili kutoa mapumziko kwa wachezaji hao baadhi ili waweze kukipa kikosi nguvu kuelekea mechi hiyo kubwa.
Kazi ya ziada itahitajika kwa Yanga ukizingatia katika mechi zake mbili za kwanza imeambulia alama moja pekee baada ya kupoteza dhidi ya MC Alger ya Algeria na Rayon Sports ya Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment