July 15, 2018


Baada ya kukamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wake, Deus Kaseke, uongozi wa Singida United umeeleza kutokuwa na shida yoyote na Yanga juu ya kumsajili mchezaji huyo.

Mkurungenzi wa klabu hiyo kutoka Singida, Festo Sanga, amesema tatizo ambalo wanalo baina yao na Yanga kwa sasa ni kuhusiana na usajili waliofanya kwa Fei Toto.

Sanga ameeleza kuwa kuna mkanganyiko mkubwa kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo ambaye amesema walikuwa wameshamalizana kila kitu mbele ya Mwanasheria.

Lakini kati hali ya kushangaza Toto ameibukia Yanga na kutambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na aliyekuwa mchezaji wa Majimaji, Jaffary Mohammed.

Sanga amefunguka kuwa watakula sahani moja na Yanga dhidi ya Toto huku akieleza hatima yake itamalizwa na bodi ya ligi pamoja na TFF.

5 COMMENTS:

  1. SAWA IKIWEZEKANA UTAPELI WA MCHEZAJI HUYU UKOMESHWE KWA SINGIDA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI FEDHA ZAO NI WIZI

    ReplyDelete
  2. Habari za kuaminika ni kuwa Kijana hajapewa pesa yeyote na Singida. Wanataka kumwundia tu njama baada ya kuwakatalia.

    ReplyDelete
  3. Hii ni danganya toto tuu. Hii inshu itaishia hewani kutokana na sgd United kuwa tawi la Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si kwel tawi la Yanga kvp ......kwa huyo Lipuli tawi la Simba ??

      Delete
    2. Kama rais wa timu kapigiwa simu kaambiwa tuachie mchezaji..bado unataka ushahidi gani!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic