July 18, 2018


Na George Mganga

Yanga imeshindwa kuuweza mziki wa Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuambulia kichapo cha mabao 4-0.

Mchezo huo uliopigwa jijini Nairobi usiku huu umeshuhudia Gor Mahia wakipachika mabao yao kupitia kwa Jacques Tuyisenge, Ephram Guikan aliyefunga mawili pamoja na Mwinyi haji aliyejifunga.

Ushindi huo wa Gor Mahia unawafanya waendelee kukalia nafasi ya pili katika kundi D wakifikisha jumla ya alama 5 huku MC Alger walio kileleni wakiwa na pointi 7 wakati Rayon Sports ya Rwanda ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 2.

Yanga imekuwa timu ya kwanza ndani ya kundi hilo kuruhusu mabao 8 baada ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya MC Algeria kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa huko Algeria na Gor Mahia FC.

Kikosi hicho sasa kimejiwekea mazingira magumu zaidi kufuzu kuelekea hatua inayofuata kutokana na matokeo mabovu ambapo katika mechi tatu kilichocheza kimeambulia alama moja pekee.


6 COMMENTS:

  1. Dah wazawa tisa wenye vipaji wamecheza ...mishahara miezi hawajalipwa
    ...usajili Mali kauli ...tutapata taabu sana

    ReplyDelete
  2. Ni matokeo mabaya kwa Yanga, ni matokeo mabaya kwa nchi pia.
    Mchezo wa Nairobi umeonesha kwamba wachezaji wa Yanga ni kama hawakuwa na maandalizi. Sijaona kujituma, sijaona uwajibikaji wa pamoja kama timu, na unaona hata walipopoteza mipira hawakuitafuta, kwa ufupi ni kwamba wachezaji hawakuonekana kujali. Ni kama watu ambao walikwenda kutimiza tu wajibu wao.

    ReplyDelete
  3. Hao ndio wazawa ambao hawana uzalendo na nchi yao, bora TFF wangeongeza idadi ya mapro iwe hata 11 la sivyo tutalisikia tu hili kombe la CAF, wazawa hawajui thamani ya nchi yao walikuwa wanacheza kama wamelazimishwa, Tshishimbi peke yake ndio alikuwa anajituma.

    ReplyDelete
  4. SISHANGAI NILIWAHI KUSEMA HUKO NYUMA BENCHI LOTE LA UFUNDI, WACHEZAJI, VIONGOZI NA SYSTEM NZIMA YA YANGA NI MBOVU.....KOCHA HUYU AKIENDELEA HIVI ATAIRUDISHA TIMU NYUMA KABISA LAZIMA MKATABA UVUNJWE HARAKA SANA....NA BENCHI LOTE LA UFUNDI. KWELI KUNA SHIDA YA PESA LAKINI HATA UFUNDI UONEKANE....MCHEZAJI ANAYECHEZA NAMBA 3 LEO ANAPANGWA NAMBA 6. HALAFU NILISEMA KUWA SIO LAZIMA KUSHIRIKI MASHINDANO YA CAF KAMA WACHEZAJI, TIMU KWA UJUMLA HAIANDALIWI, POSHO HAKUNA, MOTISHA HAKUNA, SIO LAZIMA KUSHIRIKI....AU KAMA VIPI MKOPE FEDHA BENKI MUIANDAE TIMU. PIA KUNA MAADUI WAMEPEWA AU WAMEPENYEZWA KLABUNI....ILI KUIDHOOFISHA KLABU INAANZIA KWA WAFADHILI WA YANGA (WANAOJITOLEA KUIFADHILI), TFF, THEN KWENYE UONGOZI WA KLABU, WACHEZAJI MPAKA BENCHI LOTE LA UFUNDI.....HAPA HAWA MAADUI WASIFIKIRI AIBU NI YA YANGA TU....HAPANA NI AIBU YA TAIFA..

    ReplyDelete
  5. Hamna. Yanga walikosea kujitoa kwenye Kagame. Hata kama wangefungwa lakini ingewajenga kifiziki na kitimu pia. Jana wengi wa wachezaji walionekana kama hawana nguvu na pumuzi, sasa wangechezaje na timu ambayo imeimalika kimazoezi na kuwa bora kwa kila mchezaji? Yanga wajipange na kwa kikosi kile hawawezi kushinda hata mechi moja. Wachezaji bado sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic