July 19, 2018


Wakati ikielezwa kuwa beki ambaye bado hajasaini mkataba mpya na klabu ya Yanga, Kelvin Yondani kutajwa kuelekea upande wa pili, uongozi wa Simba umeibuka na kutoa tamko.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hizo akieleza kuwa ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe.

Manara amesema Yanga wamemua kuvujisha taarifa hizo wenyewe akisema wanajichanga kusaka pesa ili baadaye wakishamsajili waje kusema wameipiga bao Simba.

Ofisa huyo ametamba kwa kusema hawamuhitaji Yondani wala hawana mpango naye tofauti na taarifa zilivyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa Simba ipo kwenye harakati za kumalizana naye.

"Ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe, wameamua kuvujisha taarifa hizo makusudi wasake pesa kisha wakija kumsajili waseme wameipiga bai Simba. Sisi hatumuhitaji wala hatuna mpango naye" alisema Manara.

4 COMMENTS:

  1. HAJI ASANTE UMEIWEKA SAWA HABARI HIYO

    ReplyDelete
  2. Yanga pambaneni na hali yenu.. .mtapata taabu sanaa

    ReplyDelete
  3. Umeeleweka sasa Yanga wapambane na hali yao

    ReplyDelete
  4. lakini hat DILUNGA TULISMEA HATUNA MPANGO NAYE ATI TUNA VIUNGO WENGI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic