Klabu ya Yanga, imewakata wachezaji wake wapya watatu iliowasajili kwa ajili ya kucheza mechi na Gor Mahia ya Kenya ikiwa ni Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) kutokana na majina yao kucheleweshwa.
Yanga, Julai 18, mwaka huu inatarajiwa kucheza na Gor Mahia nchini Kenya katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho.
Nyota ambao Yanga imewakata dakika za mwisho ni Mrisho Ngassa aliyetua akitokea Ndanda, Deus Kaseke aliyetokea Singida United na Mcongo Heriteir Makambo.
Chanzo kutoka ndani ya Yanga kilisema kuwa wachezaji hao wameondolewa kwenye mechi hiyo ya kwanza dhidi ya Gor Mahia lakini watakuwepo kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Wakenya hao utakaopigwa Julai 29 nchini hapa.
“Ngassa, Kaseke na Mcongo wameondolewa kwenye mechi yetu na Gor Mahia, hivyo hatotasafiri nao kama tulivyopanga awali kutokana na majina yao kuchelewa lakini mechi ya marudiano watakuwepo,” kilisema chanzo hicho.
UDHAIFU MWINGINE UNADHIHIRIKA WA UONGOZI HUU
ReplyDeleteUDHAIFU MWINGINE UNADHIHIRIKA WA UONGOZI HUU
ReplyDelete