July 15, 2018




Ikiwa baada ya ufanikiwa kuizidi ujanja Simba katika usajili wa kiungo wa JKU ya Zanzibar, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, Yanga wametamba kuwa hicho ni kisasi baada ya mnyama kumsajili mshambuliaji wa Lipuli FC, Adam Salamba.

Yanga juzi ilimsajili kiungo huyo ambaye alidaiwa kusaini Singida United mkataba wa awali kabla ya Wanajangwani kumpa mkataba wa miaka mitatu na kumtam-bulisha rasmi.
Awali, Yanga ilimtaka Salamba na ikapeleka barua Lipuli, lakini timu hiyo ya Iringa ikawatolea nje na kumuuza Simba kwa dau la Sh.milioni 40.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema Simba hawatakiwi kuumia baada ya kumkosa Fei Toto kikubwa wajikaze kama wao walivyojikaza baada ya kumkosa Salamba.

Nyika alisema, huo ndiyo mwanzo wa maumivu kwa Simba, hivyo wajiandae kwani ndiyo kwanza usajili wameanza kwa kumsajili Fei Toto, Jaffary Mohamed wa Majimaji na Mohamed Issa ‘Banka’ aliyetokea Mtibwa Sugar.

“Tunafa-hamu taarifa za Simba kutaka kumsajili Fei Toto muda mrefu, lakini tulifanikiwa kuvuruga mipango hiyo ya usajili kwa kuhakikisha tunamuweka katika mikono salama mapema kabla ya kwenda popote kusaini.


“Nilisema tangu awali, sisi tuliumia kwa Salamba pekee na siyo kwa hao wengine akina Wawa (Pascal) ambao hawakuwa katika mipango nao, lakini yeye Salamba alikuwa katika mipango yetu.

“Alivyokwenda Simba tulisikitika sana, lakini sasa hivi ni zamu yetu kulipa kisasi kwao kwa kumsajili mchezaji waliyesumbuka naye siku nzima wakimtafuta kwa ajili ya kumsajili huku akiwa kwenye mikono yetu salamu kabla ya kumpa mkataba wa miaka mitatu Yanga,”alitamba Nyika ambaye mbwembwe zake huwakosha mashabiki wa Yanga. 

3 COMMENTS:

  1. Hahaaaaa unajikosha kaka usajili unaoufanya mbona wala haushtui kabisa we pambana na singida si Simba hi habari nyingine kabisa.

    ReplyDelete
  2. Yanga husikeni na yenu....mnatakiwa kumalizana na wachezaji wenu wasaini mikataba mipya msifuatilie ya Simba....wao wanashughulika na Timu yao ili kuifanya iwe bora kwenye mnashindano ya kimataifa na wanasajili vikosi zaidi ya viwili vilivyo na uwiano sawa kwasababu wana malengo...Nyie mnakabiliwa na CAF sasa hivi mjikite kuwapa mikataba wachezaji na kuwaongeza foreign players wenye uwezo, muwe na vikosi zaidi ya viwili vyenye ubora wa kushindana katika ligi na mashindano mengine.......KUNA MAADUI NDANI YA YANGA MNAJUANA NYIE WENYEWE NILISHASEMA KUNA SINTOFAHAMU AMBAYO MNAJARIBU KUIFICHA FICHA, MFICHA MARADHI MARADHI MAUTI HUMUUMBUA....HATA HUYO MANJI KAMA ANA HELA MBONA HAWALIPI WACHEZAJI WANAOIDAI FEDHA KLABU???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeshauri vizuri. Kutaka kushindana na Simba kwenye kusajili wachezaji hakuna tija. Yanga shughulikeni na mambo yenu na Simba washughulike na yakwao.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic