Yanga itakuwa inacheza mechi hiyo ya mkondo wa pili baada ya ule wa kwanza kuambulia kichapo cha mabao 4-0 huko Nairobi, Kenya.
Kuelekea mechi hiyo, beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul, amesema wamejipanga vilivyo kupambana na Gor Mahia ambao wamekuja na mziki kamili wa wachezaji wao.
Abdul amefunguka na kusema Gor Mahia ni timu ya kawaida na katika mechi zote ambazo timu hiyo wamekutana na Yanga ameeleza kuwa haikuwa na kikosi kamili na ndiyo maana waliweza kufungwa.
Abdul anaamini kuelekea mechi ya kesho watapata matokeo kutokana na kikosi kujumuisha wachezaji muhimu tofauti na mechi ya kwanza iliyofanyika huko Nairobi wiki moja nyuma.
Mbali na wachezaji muhimu kuwepo, Abdul amesema pia namna mazoezi waliyofanya yatawasaidia kwani Kocha wao Mkuu, Mwinyi Zahera amefanyia mapungufu kadhaa yaliyojitokeza katikA mechi ya awali.
"Gor Mahia siyo kwamba ni timu ya kutisha vigogo, mechi zote tulizocheza nao hawajaikuta Yanga ikiwa na kikosi chake chote, kwa mazoezi tuliyojianda wiki hii naamini tutaondoka na ushindi kesho" alisema.
Yeah ni vizuri kujipa moyo kuliko kufa kikondoo
ReplyDeleteKLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..
ReplyDelete