July 23, 2018


Beki wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy ameshtukia mtego unaofanywa na viongozi wa timu hiyo na kutamka kuwa kamwe hawatampata baada ya kuwashtukia.

Kessy ni kati ya wachezaji waliomaliza mikataba ya kuendelea kuichezea timu hiyo mwishoni mwa msimu huu na kuanza mazungumzo ya kuichezea timu hiyo.

Beki huyo hivi karibuni ilielezwa kutimkia Klabu ya Nkana FC ya nchini Zambia katika msimu ujao baada ya kutakiwa na timu hiyo.

Kwa mujibu wa Championi Jumatatu, Kessy alisema ujanja wanaotaka kuufanya viongozi wa timu hiyo ni kutaka kumfanyia usajili dakika za mwisho kabla ya dirisha kufungwa ikiwa ni kwa dau dogo wakiamini hatakuwa na sehemu ya kwenda.

“Ujanja wanaotaka kuufanya viongozi nimeshaushtukia wa kutaka kunikurupusha kusaini ikiwa ni siku chache baada ya usajili kufungwa kwa dau wanalolitaka wao.

“Mimi nitasaini Yanga kwa dau ninalolitaka ambalo tayari nimewapatia kama hawatakuwa tayari kunipa hiyo hela basi, nitaondoka zangu kwingine ikiwezekana hata kurudi Mtibwa Sugar,” alisema Kessy.

5 COMMENTS:

  1. Hiyo ni mikosi anayoipata baada ya kuondoka Simba Sc kwa nyodo na matusi..Bora urudi Mtibwa Suga r ukaaanze upya..Ngómbe avunjikapo guu hurejea zizini

    ReplyDelete
  2. Duh hiyo kali na kwa kweli na mie sitamsahau na mapicha ya pozi kule Uturuki.

    ReplyDelete
  3. Mimi na mshauri angebakia yanga tu alipopazoea. Kessy sio beki mzuri sana, kwanza umbo lake dogo, na mwepesi sana kucheza rafu na kupigwa kadi pindi anapozidiwa maarifa. Akienda Nkana uajue atapata taabu sana kupata namba. Kama anabisha ajaribu mutakuja niambia hapa hapa

    ReplyDelete
  4. Kwa mimi naona bora arudi mtibwa maana hakuna namna

    ReplyDelete
  5. 'ikiwezekana hata kurudi MTIBA SUGAR'???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic