KISA SIMBA, IKULU YAWAFUATA AZAM FC TAIFA
Na George Mganga
Baada ya kuutwaa ubingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CRCAFA KAGAME CUP, uongozi wa Azam FC umepokea simu kutoka Ikulu ikiwapa pongezi kwa kutetea taji hilo.
Azam wamefanikiwa kulitetea kombe la KAGAME kwa kuwafunga Simba juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mabao 2-1.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga, amesema wamepokea simu kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyopigwa na Gerson Msigwa ikiwapa pongezi hizo.
Aidha, mbali na simu kutoka Ikulu, Azam wamepokea simu pia kutoka kwa Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Razalo Mambosasa, aliyetoa pongezi zake pia kwa timu ya Azam.
Ikumbukwe Azam ilichukua ubingwa huo pia mwaka 2015 ikiwa inaanza kushiriki mara ya kwanza kwa kuwafunga Azam FC mabao 2-0 mechi ikipigwa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment