July 7, 2018
Hatimaye Real Madrid imeweka wazi kuwa iko tayari kumuachia Cristiano Ronaldo kwenda Juventus.

Lakini imetaja dau la euro milioni 150 tofauti na awali, wengi waliamini dau litakuwa euro milioni 100.

Gazeti la Marca la Hispania, limeeleza baada ya kikao chao, Madrid wamekubaliana kwamba kama zitapatikana euro milioni 150, Ronaldo ataruhusiwa kuondoka.

Kumekuwa na gumzo kubwa kuhusiana na Ronaldo kama ataondoka au atabaki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV