July 14, 2018


Kocha aliyewahi kukinoa kikosi cha Yanga, Mseribia, Kostadin Papic, imeelezwa yupo nchini Angola kwa ajili ya kusaka kibarua cha ukocha.

Papic yuko nchini Angola kwa ajili ya kuomba kibarua cha kuifundisha timu ya taifa hilo ambayo ilishindwa kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka huu huko Urusi.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Angola, imeleezwa uongozi wa timu ya taifa hilo upo kwenye mchakato wa kupata Kocha mpya atayeweza kuisuka upya timu hiyo ili kuirejeshea makali yake kwenye mashindano ya kimataifa.

Papic ameeleza kuwa mazungumzo na uongozi wa juu wa timu hiyo unaendelea huku makocha wengine wakiwa pia kwenye harakati za kutaka nafasi hiyo ili kuanza kibarua siku za usoni.

Kocha Papic ambaye aliwahi kuifundisha Yanga mwaka 2002 amesema anajiamini anaweza kuifundisha timu yoyote kwasababu ana uwezo huo na imeelezwa kama atapata kibarua hicho atakitendea haki.


2 COMMENTS:

  1. Tutabaki kutangaza makocha wa timu za Taifa za wenzetu tu kila siku, hata wakati wa kuja kutangaza wa kwetu basi bora hata asingetangazwa kwa kuwa siku zote wahusika kama vile hawajui makocha wanapatikana wapi? Miaka kadhaa sasa Taifa Stars imekosa kocha mwenye sifa.
    Karia na wasaadizi wake hawatakiwi kitia pamba masikioni na kujifunga vitambaa vya giza usoni ili wasione maoni ya wadau wanaowatakia mema katika uongozi wao. Watu wanapokosoa au kutoa maoni yao juu ya Taifa Stars huwa hawana bifu au donge la roho na wao bali ni kuwatakia mafaniko. Tuwe wazi kabisa linapokuja suala la makocha kwa nchi zetu za kiafrica basi hakuna aina ya makocha duniani kote wanaoendana na mifumo yetu isipokuwa Vishoka yaani Makocha kutoka Eastern Europe au Ulaya ya mashariki hasa nchi asili zizokuwa Yugoslavia, Croatia miongoni mwao hata ukija ukikosea kumpata mpolandi basi hata kuangusha. Makocha wao siku zote huwa makocha wa kazi na wanafuu wa gharama na wenye kokopi kirahisi mazingira ya kiafrica. Hata hao simba wanajitoa fahamu na kujitafutia harama za bure kwa makocha wa ulaya magharibi wanatakiwa kurudi yena Ulaya ya mashariki na kutafuta kocha wa maana watampata kwa bei nafuu na wataridhika. Taifa Stars wakati wa kuwa na kocha umefika na lazima tuwe na kocha wa viwango sio majina.

    ReplyDelete
  2. Naunga mkono hoja yako kwa asilimia Mia.Makocha wa viwango na bei nafuu wako Serbia,Croatia,Rumania,Poland na hata Brazil

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic