July 14, 2018


Na George Mganga

Kocha wa Gor Mahia FC, Dylan Kerr, amelishauri Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuwa mashindano ya KAGAME yatakayofanyika mwakani yasiwe na kiingilio.

Kerr ambaye timu yake imemaliza mashindano hayo jana katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga JKU mabao 2-0, ametoa ushauri huo ili mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.

Kocha huyo ameeleza hayo akisema KAGAME ya mwaka huu haijafana kutokana na mechi zao nyingi walizocheza kukosa mashabiki hivyo ni vema kama yakafanyika bila kiingilio mwakani itakuwa vema zaidi.

Uwepo wa mashabiki wengi Kerr anaamini unatia hamasa kubwa kwa wachezaji kujituma kwa nguvu zote Uwanjani kutokana na mchango wao mkubwa wa kushangilia, kitu ambacho kinatia morali kwa wachezaji.

"Ni vema zaidi KAGAME ijayo ikafanyika bila kiingilio ili mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanjani sababu wanaleta hamasa kubwa kwa wachezaji, sioni haja ya kuweka kiingilio sababu yanakosa ladha" amesema Kerr.

Fainali za KAGAME zimemalizika jana kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC na kufanikiwa kuutetea ubingwa huo baada ya kuutwaa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 wakiifunga Gor Mahia FC kwa mabao 2-0.

KUHUSU SIMBA NA KAHATA

Wakati Kocha Kerr, amezidi kufunguka na kusisitiza juu ya suala na Simba kumtaka kiungo wake Francis Kahata, akiwataja kutum ofa ili wamalizane na mabosi wake.

Kerr ambaye amekuwa akionekana anamtegemea zaidi mchezaji huyo, amesema hatoweza kuruhusu aondoke huku akiwaonya Simba kutaka kumsajili kinyemela.

Simba wamekuwa wkihusishwa kumtaka kiungo huyo ambaye pia alikuwepo hapa nchini na kikosi cha Gor Mahia kwa ajili ya mashindano ya KAGAME.

Kutokana na tetesi hizo, Kerr amewataka Simba kuwasiliana na viongozi wa juu wa Gor Mahia ili wafuate taratibu rasmi za kumsajili na si kumvizia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV