MASHABIKI YANGA WAPINGA ONGEZEKO LA WACHEZAJI WATATU KIMATAIFA NCHINI, SABABU WAELEZA
Baadhi ya mashabiki walio wengi katika klabu ya Yanga wamepinga ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka saba mpaka kumi baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha suala hilo.
Julai 12 2018 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilipitisha kanuni za kuruhusu usajili wa idadi ya wachezaji 10 wa kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao watakaoweza kutumika wote kwa wakati mmoja.
Kutokana na maamuzi hayo, mashabiki wengi wa Yanga wamepingana na maamuzi hayo na hii ni kutokana na klabu yao kuyumba kifedha kipindi hiki.
Mashabiki hao wengi wameonekana kuandika mitandaoni wakilalamika juu ya suala hilo wakiamini timu yao haiwezi kusajili wachezaji wazuri wa kimataifa kutokana viongozi wa timu yao kukabiliwa na uhaba fedha.
Lakini wale baadhi wa upande wa pili ambao ni Simba wameonekana kuchekelea kutokana na timu yao kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji, na kumkabidhi tajiri kijana na bilionea, Mohammed Dewji, wakiamini klabu itasajili mchezaji yoyote yule kwa sasa.
Ukiachana na mitandaoni, katika vijiwe vya maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam baadhi yao wamekuwa wakipinga huku wengine wakisifia wakiamini italeta ushindani mkubwa.
Walioamini ushindani utakuwepo wameeleza ni kutokana na wazawa watapaswa kujituma zaidi Uwanjani ili kujiwekea namba kwa lengo la kushindana kiuwezo na wageni, hivyo itakuwa ni changamoto kwao kujipanga zaidi ili kufanya vizuri.
Suala hili la kuongezwa kwa wachezaji watatu kuwa kumi kwa usajili wa wachezaji wa kigeni limekuwa na maoni tofauti. Angalau Yanga wao wanasema wazi Kwamba timu yao haina uwezo wa kushindana katika kusajili wachezaji wa kigeni. Lakini nilishangazwa sana na Maoni ya baadhi ya watu ambao kimtazamo wanauwelewa mpira hapa Tanzania kupingana na uamuzi huo wa TFF ya kuongeza wachezaji wa kigeni. Wanaolalamika wamo makocha wazoefu wa mpira,wachezaji wastaafu na wachambuzi wote wanamadai ya kuihofia Taifa Stars? Lakini cha ajabu mfumo huu wa sasa ndio zalio la Taifa Stars yetu tulionao. Mimi naona hawa wadau wanaolia na kuongezwa kwa idadi ya wachezaji wa kigeni wanakosa point kwani wao walikuwa ndio wawe wa kwanza wa kuunga mkono hili suala kwani wachina wanaamini mtu kufikwa na changamoto ni bahati na wachezaji wetu kuja kupata ushindani kazini kwao ni bahati pia. Hakuna cha kusema kuwa hakujaandaliwa mfumo maalumu wa kukabili ongezeko hilo la wachezaji wa kigeni kwa wachezeji wazawa. Wadau wanatakiwa kutumia nguvu zao nyingi za kulalamikia ongezeko hilo la wachezaji wa kigeni kuwafunda wachezaji wazawa jinsi ya kukabiliana na ushindani unaokuja na kuongeza viwango vyao badala ya kuwajaza hizi kasumba za hofu na chuki kwa wachezeji kigeni.
ReplyDeleteRaisi Karia na TFF hawatakiwi kutetereka na maneno ya waoga. Mfano Raisi Magufuli alipotangaza elimu bure wapinzani walipinga sana kwa madai mbali mbali,ooh huo ndio mwisho wa kiwango bora cha elimu Tanzania, ooh anania ya kuuwa elimu,ooh hataweza huyo huu mpango utafeli tu. Lakini leo tunashuhudia shule ya serikali inaongoza kwa ubora nchi zima ni kipindi kifupi tu, tena sio shule ya Dar au Arusha au Kilimanjaro ni kibaha?
Kama watanzania wote tutaacha uoga wa kipumbavu na kufuata uthubutu wa mueshimwa Rais Magufuli kwa vitendo basi Tanzania inawezekana ikawa miongoni mwa nchi za ajabu kwa maendeleo kwa kila sekta na kuishangaza dunia.
Yes, ni kweli kabisa. Hapa kinachoonekana baadhi ya WA Tanzania ni waoga kupitiliza. Tuondoe woga na tutumie fursa ya kujifunza vitu toka kwa wageni na hii itatufanya tubadili mtizamo,tujipime na kuongeza juhudi, bidii. Mwisho WA siku itatufanya kuzidi kuimarika na kukua zaidi. Shida wengi hatujui kuwa ktk maisha mbali na soka changamoto watu huwa tuna develop toka hatua moja kwenda nyingine ni baada ya kukumbana na changamoto kadhaa na kukabiliana nazo, hill linapelekea kukua. As hao wanaopinga hawako tayari kwa hili, wanaona tulipoishia panatosha. Ni vema ss waone kuwa hii inaweza kuwa ni changamoto, hivyo waumize vichwa( kwa ushauri, n.k)ni namna gani ya kuikabili na kupata matokeo chanya.
Deleteumeongea vizuri sana
DeleteWazo la wachezaji 10 wa kigeni sio baya ila ni kanuni za utekelezaji wake ndio tatizo.
ReplyDeleteSHIDA YA YANGA NI NAFASI ZIFUATAZO NAMBA 5, 6, 7, 9, 11, MNATAKIWA MSAJILI BEKI WAWILI WA KUTOKA NJE, NA KIUNGO MKABAJI SIO WAKINA MAKAPU NA ANDREW VINCENT WANAOKABIA MACHO!!! MBONA MNATAFUTA WA BEI CHEE!!!...TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WA MAANA KWA NAFASI ZA NAMBA 5, 6, 9, 7 NA 11.......NAANZA KUMWAMINI TARIMBA KUWA UONGOZI WA YANGA NI WA UBABAISHAJI NA WASANII TU, KUWADANGANYA WAPENZI WAO.....NA KAMA UONGOZI HUU UTAENDELEA NA MTINDO HUU....UBINGWA UTAKUWA WA SIMBA, AU AZAM.....SIDHANI KAMA WACHEZAJI DIZAINI HIZI WANAWEZA WAKASHINDANA NA TIMU KAMA SIMBA AU AZAM ZENYE VIKOSI KIPANA AMBAPO UNAWEZA UKAPATA HADI VIKOSI 2......TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WENYE UWEZO WA HALI YA JUU WATAKAOLETA USHINDANI....
ReplyDeleteHUYO KOCHA ANAWALOSTISHA NA KUWASHAURI VIBAYA!! KAMA MNATEGEMEA KUSHINDANA NA KUTWAA UBINGWA KWA WACHEZAJI DIZAINI HIZI!!!!...YANGA INAKUWA KAMA LIPULI AU PRISON KWA USAJILI WA WACHEZAJI KAMA HAWA!
Yanga majanga kwanini inashowing off usajili wa wachezaji wapya wakati kuna rundo la wachezaji wamegoma kwa kuidai timu? Kama lengo ni kuidodesha Simba kuwa yanga na wao wanafanya usajili basi huo ni ulimbukeni wa kijinga kabisa kwani Simba hata Azam mwenye hali yake amekaa mbali kabisa kutaka kushindana na Simba. Yanga wasipokuwa makini watapata tabu sana mwaka huu. Sina hakika na wengine kama dante lakini yondani alishasaini simba zamani sana badi kutangazwa tu.
ReplyDeleteInashangaza leo wanayanga wanalalamikia kuongenza wachezaji wa kigeni ktk ligi yetu wakati wanajiita wa kimataifa.kwa hali ilivyo Yanga bado wanachama hawajitambui na mabadiliko ya kuendesha klabu kwa mifumo sahihi ya kibiashara kwani soka ni pesa.Hata ndondo cup ni pesa.TFF yenye nguvu inahitaji pesa kwa kuboresha ligi zake na kuongenza wachezaji wa kigeni ni mbinu mojawapo ya maboresho na yenye tija kwa wanasoka wetu kuwa wanapaswa kupambana ili wapate mkate wa kuendesha maisha yao na familia.Simba haiwezi kufanikisha mfumo wa uendashaji wa klabu kwa kupeleka timu kushindana klabu bingwa Africa na yenye wachezaji wenye viwango duni.Simba iko sasa kibiashara zaidi inahitaji wachezaji wa kiwango ili kupandisha brandy ya Simba kuwezesha Hisa ziwe na thamani.Wanayanga pambaneni na hali yenu ..achaneni na mawazo mgando kuwa bila fulani basi klabu haiwezekani kuendeshwa.Ni hoja yangu hivyo tafadhali sihitaji matusi.
ReplyDeleteSiyo lazima kujaza nafasi zote 10!! Yanga sajilini mnaowaweza, hata 3 wanatosha wa kigeni wengine wawe wazawa ili muwe na wachezaji wengi wa kuitwa Taifa Stars! hamuoni sifa!!
ReplyDelete