July 23, 2018





Mwanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji maarufu kama MO Dewji amewaombea dua Yanga kupita katika matatizo yaliyopo sasa.


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Dewji ambaye ni mfanyabiashara bilionea amesema anatamani kuona Yanga imara inayoongeza ushindani kati yake na Simba.


Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba. Tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars. Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya.”


Amesema anaamini kama Yanga itakuwa imara, basi Simba ina nafasi ya kupata ushindani na pia kupambana.


Lakini akasisitiza, kwamba Yanga na Simba zinapokuwa imara basi kuna nafasi nzuri kwa timu ya taifa, Taifa Stars kufanya vema.


Yanga iko katika migogoro mikubwa ya uongozi huku makundi yakiendelea kujijenga ndani ya klabu hiyo kila kunapokucha.

1 COMMENTS:

  1. Huo ndio ungwana.Tajiri mstaarabu.Lkn mnakumbuka upande wa pili enzi hizo Tajiri wao alisema ana uwezo wa kuipoteza Simba na akanunua wachezaji wote na kuwalipa mishahara yao bila kucheza.Na mashabiki wao wakaendelea kutoa kejeli lukuki tukashindwa kupumua.Binadamu tujifunze kuweka akiba ya maneno.Bado nawapa hongera kina Hans Pope, Rage, Evans, Haji Manara, Kilomoni, Mtawali,Kaburu na viongozi wote wa Simba waliopitia kipindi kile kigumu pamoja na wanachama, mashabiki na bila ya kumsahau Waziri Mwakiyembe kwa kilichoifikisha klabu ya Simba kwenye mabadiliko haya ya mfumo wa uendashaji wa klabu kisheria kwa hisa 51% za klabu na 49% mwekazaji MO japo kwa kila jambo mwanzo mgumu lkn tumethubutu na muhimu kuenedlea na mshikamano tulioanza nao....InshaAllah

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic