July 23, 2018

MSEMAJI WA TFF, CLIFFORD NDIMBO



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha vilabu vya Ligi Kuu,Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ambavyo havijafanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa TFF FIFA Connect kufanya usajili wao.

Vilabu ambavyo bado havijafanya usajili wawasiliane na TFF kama kuna msaada wowote wanahitaji ili kukamilisha usajili wao.

Dirisha la Usajili litafungwa Alhamis Julai 26,2018 na TFF inasisitiza hakutakuwa na muda wa ziada katika usajili.

Timu ambayo itashindwa kukamilisha usajili haitaruhusiwa kushiriki Ligi ya msimu ujao wa 2019/2019.

Vilabu ambavyo havijafanya usajili mpaka sasa

LIGI KUU:
Ruvu Shooting, Mbeya City,Tanzania Prisons,Mtibwa Sugar, Mwadui, Kagera Sugar, Alliance, Lipuli, African Lyon, KMC na Azam

FDL:
Ashanti United, Boma FC, Friends Rangers, Green Warriors, Kiluvya United, Majimaji FC, Mashujaa FC, Mawenzi Market, Mbeya Kwanza, Mgambo Shooting, Njombe Mji, Pamba FC, Dar City na Polisi Tanzania

SDL:
Area C United, Changanyikeni, Cosmopolitan FC, Kumuyange FC, Gipco FC, Mirambo FC, Madini FC, Mkamba Rangers, Mvuvumwa, Polisi Dar, The Mighty Elephant, Toto African, Villa Squad, Majimaji Rangers, Mtwivila City, Kasulu Red Star na Sahare All Stars

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic