Aliyekuwa beki wa kushoto wa mabingwa wa Tanzania, Simba, Jamal Mwambeleko ametua Singida United.
Singida United imempa Mwambeleko mkataba wa Mwaka mmoja na tayari amekabidhiwa jezi yake kwa ajili ya msimu ujao.
Mwambeleko amejiunga na Singida United akitokea Simba SC ambako alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja.
Maongezi mazuri kati ya Simba na Singida United yamefikia hatua ya mchezaji huyo kuelekea kwa walima alizeti kwa kukipiga msimu ujao.
Mwambeleko alijiunga na Simba akitokea Mbao FC, lakini akashindwa kabisa kuonyesha cheche katika kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi huku Asante Kwasi akionekana kuitendea haki namba tatu kwa kusaidiana na Mohammed Hussein 'Tshabalala'.








Ni bora akakuze kipaji chake kuliko kukaa benchi tu eti mradi anapokea salary
ReplyDelete