July 22, 2018


Mshambuliaji Donald Ngoma amefunga safari hadi kwa mhubiri maarufu wa nchini Nigeria, TB Joshua ili kuombewa goti lake.

Ngoma ambaye sasa amejiunga na Azam FC amekuwa akisumbuliwa na goti kwa muda mrefu, ingawa kumekuwa na habari mkanganyiko.

Lakini safari hii amefunga safari hadi Nigeria katika kanisa la Synagogue la nchini Nigeria linalongozwa na TB Joshua.


Picha zinaonyesha Ngoma akiwa jukwaani na TB Joshua ambaye baadaye anamuombea akimtaka kufungua goti lake, naye anapandisha suruali yake.


Haijajulikana kama matibabu yake yalishindikana kabisa kabla ya kuchukua uamuzi huo na Ngoma sasa ni mchezaji wa Azam FC baada ya kuondoka Yanga.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic