July 7, 2018


Shabiki kija­na amepoteza maisha baada ya timu ya taifa ya Argentina kufun­gwa na Ufaransa na kuondolewa katika Kombe la Dunia (World Cup), wikiendi iliyopita.

Shabiki huyo ali­yefahamika kwa jina la Monotosh Halder mkazi wa Habibpur, Wilaya ya Malda nchini India, alipata mfadhaiko mara baa­da ya timu hiyo inayoon­gozwa na Lionel Messi kufungwa mabao 4-3 huku yeye akiwa shabiki mkubwa wa Messi.

Mara baada ya mch­ezo huo, Monotosh, 20, alishindwa kula usiku, akaenda kulala, asubuhi yake wakakuta akiwa amefariki. Polisi hawajaweka wazi sababu za kifo hicho, lakini ndugu zake wote walisema hakuwa akiumwa.

Taarifa za mtaani kwake zinaeleza kuwa aliamua kujiua baada ya kupata mfadhaiko huo wa matokeo hayo.


Baadaye taarifa ya polisi ilisema: “Tunaendelea na uchunguzi na inaonekana ni kama alijiua mwenyewe mara baada ya Ar­gentina kuondolewa kwenye Kombe la Dunia.”
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV