July 7, 2018


Mshambuliaji mpya wa Simba, Meddie Kagere, amefungukia mabao yake mawili ambayo ameyafunga kwenye michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kagere raia wa Rwanda, amejiunga na Simba hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili ambapo mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi mbili za Kagame kati ya tatu ambazo timu yake ya Simba imecheza mpaka sasa.

Katika mechi hizo dhidi ya APR ambayo Simba ilishinda mabao 2-1, Kagere alifunga bao la ushindi kwa penalti, kisha akafunga kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Singida United.

Akizungumzia mabao hayo, Kagere ameliambia gazeti la Championi kuwa: “Hii inatokana na wachezaji wenzangu juu ya kusaidiana tunapokuwa uwanjani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwangu kufunga.

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuendelea kufunga mabao kama nilipotoka. Kwa sasa siwezi kuanza kusema kwamba ninataka kuwa mfungaji bora wa michuano hii, tusubiri kuna mechi nyingi mbele, lakini pia Mungu ndiye anayejua kila kitu, nitaendelea kumuomba anisaidie katika hilo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic