SIMBA NAO WATOA TAMKO LAO JUU YA TOTO KUSAINI YANGA NA SINGIDA KWA SIKU MOJA
Uongozi wa klabu ya Simba umetolea ufafanuzi juu kiungo mchezaji Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' ambaye usajili wake umezua gumzo jana kwa kujiunga na Yanga akitokea JKU kwa kusaini miaka miwili.
Baada ya Toto kuhusishwa kuhitajika na Simba, Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema klabu yao haikuwa na mipango ya kumsajili mchezaji huyo kutokana na kujaza viungo wengi.
Manara ameeleza kuwa Simba ina wachezaji wengi viungo akisema usajili wa mchezaji huyo kwenda Yanga usihusishwe na Simba kwakuwa hawakuwa na mpango naye.
Toto ametambulishwa Yanga jana ikiwa ni baada ya masaa kadhaa kupitwa kutangazwa na uongozi wa Singida United kuwa wameingia naye mkataba wa miaka mitatu.
Usajili huo ulikuwa gumzo kubwa jana baada ya Yanga kuitisha kikao na wanahabari majira ya saa 10 jioni ili kumtambulisha Toto ambaye alikuwa pamoja na wakala wake na kuleta sintifahamu ikiwa ni baada ya Singida kumtangaza pia.
Wachezaji wetu awajielewi
ReplyDeleteFei Toto kachagua sehemu sahihi kwa mustakabali wa soka lake! Pale kwetu Simba angeua kipaji kwani hana nafasi ya namba mbele ya viungo mafundi walioko pale. Yanga au Singida sawa hana mpinzani.
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeleteKwani Manara bila kuitaja Yanga siku yake aiendi vizuri
ReplyDeleteManala nae no binadamhuendayanga inampa furaha
ReplyDelete