Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini Julai 16 Jumatatu kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia, Julai 18 jijini Nairobi.
Yanga inashika mkia katika kundi lao kwa kuwa na pointi moja huku USM Alger ikiongoza kwa kuwa na pointi nne ikifuatiwa na Gor Mahia yenye pointi mbili na Rayon Sport ya Rwanda yenye pointi mbili pia.
Awali, Yanga ilikuwa iweke kambi ya siku chache Arusha kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo lakini imeshindikana na badala yake wanakwenda moja kwa moja.
Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe amesema: “Maandalizi yanakwenda vizuri kama inavyotakiwa na wachezaji wote wameshaanza mazoezi kuelekea mchezo huo.
“Kwa sasa sijajua ni idadi ya wachezaji wangapi watakwenda huko lakini kwa upande wangu niliona ni vyema wachezaji wote wakaenda,” alisema Hafidh.
CHANZO: CHAMPIONI
Hapo vyura ni kichapo kwa kwenda mbele
ReplyDelete