YANGA, jana iliwatambulisha nyota wawili wapya, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kutoka JKU ya Zanzibar iliyompa mkataba wa miaka mitatu na Jaffar Mohammed aliyekuwa Majimaji aliyepewa mkataba wa miaka miwili.
Mkurugenzi wa Singida United alitoa tamko kwa kusema: “Feisal tumemsaini kwa mkataba wa miaka mitatu tukiwa tumekutana naye chini ya mwanasheria na wakala wake na mchezaji mwenyewe alikubali kusaini na sehemu kubwa ya fedha ameshachukua.
“Hajasaini ‘pre contract’ kama watu wanavyosema, ile ni ‘contract’ inayotambulika na ndiyo itatumika kwenye usajili wake kama ambapo tutakuwa tumefikia makubaliano ya kumsajili pale TFF watakapoamua. “Sisi tunajua mchezaji huyu amesajili Singida United, haya ambayo yametokea kwamba amesajili Yanga ni ‘double standards’ kwa sababu linawaweka Watanzania njia panda.
“Sisi tunajua mche¬zaji huyu amesajili Singida United, haya ambayo yametokea kwamba amesajili Yanga ni ‘double standards’ kwa sababu linawaweka Watanzania njia panda. Sisi tunaamini vyombo vinavyohusika na usajili ambavyo ni Bodi ya Ligi na TFF vitaamua jambo hili kwani tumeshamalizana na JKU.”
Katika usajili huo, gumzo kubwa lilikuwa ni usajili wa Fei Toto ambaye kabla ya jana jioni Yanga haijamtan¬gaza kuwa mchezaji wao, asubuhi yake, Singida United ilimtambulisha imemsa¬jili kwa kumpa mkataba wa miaka mitatu.
Usajili huo ilikuwa kama filamu kwani asubuhi Mku¬rugenzi wa Singida United, Festo Sanga, alitangaza wamemsajili mchezaji huyo na kusambaza picha pamoja na video zinazoonyesha uthibitisho wa hicho kilicho-fanyika.
Haikupita muda mrefu, jioni Yanga ikamtambuli¬sha Fei Toto klabuni kwao ambapo katika utambulisho huo, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika ndiyo walihusika.
Mbali na Singida kutan¬gaza kumsajili Fei Toto kabla ya Yanga haijapindua meza kibabe, Simba nayo inatajwa ilikuwa ikimuhitaji
0 COMMENTS:
Post a Comment