July 14, 2018


Mshambuliaji mpya wa Simba, Mnyar­wanda, Med­die Kagere ametamba kasi hiyo ya kufumania nyavu aliyoianza kwenye michuano ya Kombe la Kagame, amepanga kuendelea nayo kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Hizo ni salamu kwa mabeki wa timu pinzani wa Yanga, Kelvin Yondani, Vincent Andrew ‘Dante’ na Azam FC, Aggrey Morris katika kuelekea kwenye msimu ujao.

Mnyarwanda huyo alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Gor Mahia ya nchini Kenya baada ya mkataba wake kumalizika ambaye hadi hivi sasa amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo minne aliyocheza ya Kombe la Kagame ambayo leo in­afikia fainali kwa Simba kucheza na Azam FC.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Kagere alisema amekuja kuichezea Simba kwa ajili ya kuipa mafani­kio pekee na siyo kitu kingine kwa kuhakikisha anaifungia mabao timu yake hiyo mpya.

Kagere alisema anafu­rahia ushirikiano mzuri aliokuta Simba kwa kuanzia kwa wachezaji, viongozi na mashabiki ambao walimpokea vizuri, hivyo amepanga kutowaangusha na kuthibitisha ubora wake kwa kuendelea kufunga zaidi.

Kitu ninachokiomba hivi sasa kutopata ma­jeraha pekee, kila siku ninamuomba Mungu nisipate majeraha kwani yataharibu malengo yangu niliyoyapanga nikiwa na Simba.

“Nguvu zangu nitazielekeza kwenye ligi kwa kuendelea kufunga zaidi mabao na katika hilo ninaamini nitafanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa ninaoupata Simba kutoka kwa wachezaji.


“Mashabiki wa Simba watarajie mengi mazuri kutoka kwangu, kwani ninawapenda sana nimekuja kuwapa furaha,” alisema Kagere.

1 COMMENTS:

  1. Simba ya kagere, Boko na Okwi tema mate chini. Hata simba wakijaliza spea nyengine ya mtu mzima wa maana maana pale mbele sio zambi kwani inaonekana akina kaheza bado wanakosa uthubutu wa akina Mbabe na fainali ya kagame imetowa majibu fasaha juu ya mechi ngumu na uwezo wa vijana wa Simba kupambana na kupata matokeo chanya hasa wale wapya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic