July 13, 2018

AFANDE CHOMODY (KULIA) AKIWA NA FEI TOTO WAKATI WA KUTAMBULISHWA YANGA.Pamoja na Simba kuweka msisitizo haitaki kuhusishwa na suala la kiungo Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, meneja wake, amesisitiza, Simba walimfuata.


Meneja Mohamed Kombo ambaye pia ni Meneja wa JKU, amesema anajua Simba walimfuata Fei Toto.

Kombo maarufu kwajina la Afande Chomody amethibitisha mchezaji wake kufuatwa na Simba na Singida United kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo.


Kiungo huyo alitamburishwa baada ya kuingia mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Kombe la Shirikisho Afrika wanayoshiriki.

“Kuanzia leo (jana) Fei Toto ni mchezaji halali wa Yanga ni baada ya Yanga kufuata kanuni za usajili wa mchezaji wangu kwa kuanza kufanya mazungumzo na wamiliki wa mchezaji mwenyewe ambao ni JKU.


“Zipo baadhi ya timu zilimfuata kwa ajili ya mazungumzo ikiwemo ikiwemo Simba na Singida United ambayo yenyewe tunasakia ilimsajili bila ya sisi kujua chochote kama wamiliki wa mchezaji huyo,”alisema Afande Chimody.


Leo, Msemaji wa Simba, Haji Manara amesisitiza kwamba watachukua hatua kama atatokea mtu kuwahusisha na suala la Fei Toto.

Manara “ametupa” mkwara akisisitiza kwamba Simba haihusiki na suala hilo na isingependa kuona inahusishwa.

4 COMMENTS:

 1. Kwahiyo ?? Huyu KOmbo tatizo. Haoni kuwa mchezaji huyo amewatapeli Singida, yeye anaona sawa tu?

  ReplyDelete
 2. SHIDA YA YANGA NI NAFASI ZIFUATAZO NAMBA 5, 6, 7, 9, 11, MNATAKIWA MSAJILI BEKI WAWILI WA KUTOKA NJE, NA KIUNGO MKABAJI SIO WAKINA MAKAPU NA ANDREW VINCENT WANAOKABIA MACHO!!! MBONA MNATAFUTA WA BEI CHEE!!!...TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WA MAANA KWA NAFASI ZA NAMBA 5, 6, 9, 7 NA 11.......NAANZA KUMWAMINI TARIMBA KUWA UONGOZI WA YANGA NI WA UBABAISHAJI NA WASANII TU, KUWADANGANYA WAPENZI WAO.....NA KAMA UONGOZI HUU UTAENDELEA NA MTINDO HUU....UBINGWA UTAKUWA WA SIMBA, AU AZAM.....SIDHANI KAMA WACHEZAJI DIZAINI HIZI WANAWEZA WAKASHINDANA NA TIMU KAMA SIMBA AU AZAM ZENYE VIKOSI KIPANA AMBAPO UNAWEZA UKAPATA HADI VIKOSI 2......TAFUTENI WACHEZAJI WA KIGENI WENYE UWEZO WA HALI YA JUU WATAKAOLETA USHINDANI....
  HUYO KOCHA ANAWALOSTISHA NA KUWASHAURI VIBAYA!! KAMA MNATEGEMEA KUSHINDANA NA KUTWAA UBINGWA KWA WACHEZAJI DIZAINI HIZI!!!!...YANGA INAKUWA KAMA LIPULI AU PRISON KWA USAJILI WA WACHEZAJI KAMA HAWA!

  ReplyDelete
 3. Pilipili msiyoila yawawashia nn? pambaneni na hali zenu la sivyo MTAPATA SHIDA SANA.

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV