July 15, 2018


Hatimaye kiama cha michuano ya Kombe la Dunia Urusi kimefikia mwisho leo kwa timu ya taifa ya Ufaransa kuweza kutwaa Kombe hilo kwa kuifunga Croatia mabao 4-2.

Mabao ya Ufaransa yamewekwa kimiani na Mario Mandzukic aliyejifunga, Antoine Griezmann aliyefunga kwa njia ya penati pamoja, Paul Pobga pamoja na Kylian Mpabbe.

Wakati huo mabao ya Croatia yamepachikwa kimiani na Ivan Perisic pamoja na Mario Mandzukic aliyesahihisha makosa yake kwa kuifungia timu yake bao la pili.

Ubingwa huo kwa Ufaransa unakuwa wa pili baada ya kuutwaa pia katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini kwao.

Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amekuwa miongoni mwa makocha watatu kutwaa ubingwa huo kama mchezaji na Kocha baada ya Mbrazil Mario Zagallo na Mjerumani Franz Beckenbauer.

Vilevile Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao manne katika fainali hizo tangu Brazil iifunge Italia 4-1 mwaka 1970.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic