VIDEO ZA MAGOLI: SIMBA NA AZAM WALIVYOTINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME
Gori Simba limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere limetosha kuipa timu hiyo ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar jioni ya jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. AZAM FC imefanikiwa kwenda Fainali Kombe la Kagame baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jamani chama langu la msimbazi vipi tena? Nasikia huyu mkongomani bado ana mkataba unaoisha mwakani mwezi wa 7. Timu yake anayoichezea sasa hivi Kiyovu Sports ya Rwanda inataka kuipeleka Simba Fifa kuilalamikia kufanya mazungumzo na kumfanyisha mazoezi mchezaji wao ambaye bado ana mkataba....Jamani ehe pamoja na kwamba tuna shida ya wachezaji wa kigeni lakini tufanyeni mambo kwa weledi kidogo tusije kuingia kwenye matatizo, na hizi pesa za mwekezaji zitumiwe vizuri sio kwa pupa. Haya mambo kama ni kweli basi Simba tutaumia kweli na mkono wa Fifa
ReplyDeleteYanga kama si watu wa shukrani kwa Simba kwa hili jambo basi ni wakosefu wa fadhila na wanaweza kupata laana. Kitendo cha simba kumngoa Kagere Gormahia kumewarahisishia kazi yanga. Hizo habari sijui yanga ilikuwa inataka kumsaji wao hakuna lolote kwani uwezo wao sasa ni wa kuunga unga. Yaani ni sawa na fala kumusudu mrembo alie ndani ya runinga.
ReplyDeleteHapa Yanga anahusika vipi? Mimi nadhani ungewauliza Kiyovu Sports ya Rwanda
DeleteHapa Yanga anahusika vipi? Mimi nadhani ungewauliza Kiyovu Sports ya Rwanda
DeleteKama Nicholasi gayan wa simba kutoka Ghana alikuwa mfungaji mahiri na fowadi matata katika ligi ya Ghana sasa ni wakati muafaka kwa benchi la ufundi la Simba taratibu wanatakiwa kumrejesha kwenye nafasi yake ya asili kwani ni mchezaji mwenye kujituma na potential ya kuwa msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji kuelekea mechi za kimataifa.
ReplyDeletetunachohitaji sasa hivi ni ubingwa wa kombe la kagame kwa kumfunga azam
ReplyDelete