July 12, 2018


Timu ya Taifa ya England imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Croatia kwa idadi ya mabao 2-1.

Katika mchezo huo, dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 na kuamuriwa kuongezwa dakika30 za ziada ili kupata mshindi wa mechi.

England walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 5 ya mchezo kwa njia ya mpira wa adhabu uliopigwa na kuwekwa kimiani na Kieran Trippier na baadaye kipindi cha pili Croatia walisawazisha kupitia kwa Ivan Perisic dakika ya 68.

Baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare hiyo, 30 zingine ziliongezwa na Croatia walizitumia vema kwa straika wake, Mario Mandzukic kuandika bao la pili kwenye dakika ya 106.

Mpaka Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo yalibaki kuwa 2 kwa Croatia na 1 kwa England.

Kutokana na England kuondoshwa leo, sasa itacheza dhidi ya Ubelgiji kusaka mshindi wa tatu Jumamosi huku Croatia ikiungana na Ufaransa kucheza fainali Jumapili ya wiki hii.

2 COMMENTS:

  1. Kweli mpira ni mchezo unaochezwa hadharani. Nimekuwa nikiangalia world cup tangia nikiwa na umri mdogo kabisa kabla hata sijaanza shule na hivi sasa nina hamsini naa miaka lakini hii world cup ni moja ya world cup yenye mambo mengi ya kujifunza. Mfanao mechi ya mwanzo kabisa ya Croatia ilimunesha kila mwenye macho ya kuona kuwa croatia wana timu yenye uwezo mkubwa kabisa wa kumfunga yeyote yule watakae kutana nae. Ufaransa hata kabla ya kombe la Dunia kuanza walikuwa washafika fainali ya mashindano hayo. Tatizo la ufaransa katika miaka ya hivi karibuni ni kocha. Inaonekana kana kwamba makocha wa ufaransa wanafuata maelekezo kutoka chama cha mpira cha nchi yao jinsi ya mpangilio wa timu. Na inawezekana mtu kama zidane mwenye maamuzi binafsi kwenye taaluma yake itamnuia vigumu kuwa kocha wa ufaransa. Anthony Mashal na kylan Mbape ni muunganiko sahihi kabisa kwenye safu ya ushambuliaji au mzoefu kama karim benzima na Elexand lacazette ni safu ya ushambuliaji yenye nguvu na vibweka. Kwanini kocha wao ana ng'ang'ania kumchezesha mshambuliaji aliefeli kama oliver Gerod? Ni kasumba ya urangi na ufaransa asilia katika timu lakini kama timu ya Taifa ya ufaransa ingekuwa ipo chini ya kocha sahihi kama vile Zidane basi timu nyengine zingepata taabu sana ila tunafurahi kuona timu stahiki kuingia fainali na tunatarajia kuona fainal tamu kabisa ya kombe la Dunia katika zama hizi ingawa wafaransa wanashindwa kuonesha kiwango chao sahihi kutokana na upumbavu wa kocha wao.

    ReplyDelete
  2. Uzito wa kocha wa uengereza kushindwa kufanya maamuzi sahihi katika wakati muafaka ndiko kuliko iangusha Uingereza leo. Harry keane alikuwa hayuko sawa na badala ya kuwa msaada kwa timu aligeuka kuwa mzigo. Angemfanyia mabadiliko mapema.Mchezaji mbishi kama Fabian Delphi hii ndio ilikuwa mechi sahihi kwake.lakini kocha ndio kocha ndie mwenye uamuzi wa mwisho wacroatia walitoa mchezaji sahihi na kuingiza mchezaji mwenye msaada na huo ndio ukawa mwisho wa story.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV