July 26, 2018


Na George Mganga

Zikiwa zimesalia saa kadhaa kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili hapa Bongo, klabu ya Yanga imeingia mkataba na wachezaji wawili kwa kusaini nao mkataba wa miaka miwili kutoka Congo.

Wachezaji hao ni mshambuliaji Heritier Makambo ambaye alitua wiki kadhaa zilizopita na kuanza majaribio kisha kocha Mwinyi Zahera kuridhishwa na kiwango chake na kuwaomba mabosi wake wamsajili.

Mbali na Makambo, Yanga pia imemalizana na kipa Klauz Kinzi Kindoki ambaye anatajwa kuchukua nafasi ya Mcameroon, Youthe Rostand baada ya kuwa na kiwango ambacho hakijaridhisha wengi katika msimu uliopita.

Usajili wa kipa huyo umefanyika ambao inaelezwa mabosi wa Yanga wapo katika mchakato wa kumpeleka Rostand timu nyingine kwa mkopo baada ya kuonesha kiwango ambacho si stahiki ndani ya timu hiyo.

Aidha, wanachama na mashabiki wa Yanga wamekuw wakiushawishi uongozi wao kwa muda mrefu juu ya Rostand wakitaka aondoshwe kutokana na uwezo wake ndani ya Uwanja kuwa mdogo.

Dirisha la usajili linafungwa leo majira ya saa 6 kamili usiku tayari kwa timu kuanza maandalizi ya msimu ujao wa ligi utakaokuwa na idadi ya timu 20 kutoka 16 msimu uliopita.

9 COMMENTS:

  1. DIRISHA LA USAJILI LIMEFUNGWA LAKINI MPAKA SASA HAKUNA WASHAMBULIAJI WA MAANA WA KIGENI WALIOSAJILIWA YANGA KOCHA ANAWAPOTOSHA HUYU.......AU NYIKA ANAIUA YANGA??

    ReplyDelete
  2. Beki wa kati wa kigeni bado pia, mapungufu ya beki, washambuliaji ndiyo yalikuwa mapungufu ya Yanga, lakini nashangaa hawajayaziba (ngoma, chirwa, mbadala wa Tambwe )

    ReplyDelete
  3. Mbona jamaa wanaonekana kama wana mawazo sana. Bila shaka wamekopwa.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. WANACHAMA WA YANGA BADO HAWAJARIDHIKA NA USAJILI HUU MAPUNGUFU KWENYE TIMU HAYAJAZIBWA HASWA UPANDE WA WASHAMBULIAJI NA, BEKI WA KATI NA KIUNGO WA ULINZI.....HILI JAMBO LINAWEZA KULETA MPASUKO MKUBWA NA DHAHAMA HAPO YANGA INABIDI WANACHAMA WAELEZWE KWANINI WACHEZAJI WA NAFASI YA USHAMBULIAJI WALIOKUJA KWENYE MAJARIBIO AU HATA WA HAPA NDANI HAWAJASAJILI. USAJILI HUU HAUJAKIDHI MAHITAHI YA TIMU......MASHABIKI WAKIGOMA KUJA VIWANJANI MSIWALAUMU....BADO HALI SI NZURI, HAKUNA HAMASA KWA MTU AKIUANGALIA USAJILI HUU...ANAYEHUSIKA NA KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI ATABEBA LAWAMA SANA NA YASIJE KUWA YALE YA SANGA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watanzania wengi huwa wanapenda kuona usajili wa Lundo la wachezaji...Yanga inachokifanya ni kuangaika kuziba nafasi za maeneo kazaa ambayo yalionekana ni pengo. Sisi tunapenda majina na si kazi ya uwanjani. Angalia uwezo wa Yusuf Muhilu...naamini ana uwezo mkubwa sana wa kuziba nafasi ya Donald Ngoma...Yupo Makambo ambae ni Mbadala wa Chirwa. Yanga sehemu iliyokuwa na mazaifu ni eneo la mbadala wa dogo Msuva ambalo lilibaki wazi kwa muda mrefu sana baada ya kufeli kwa mahadhi. Kiungo wa Ulinzi ni Tshishimbi..wakati kiungo wa ushambuliaji yupo Thabani Skalla, Faisal, Kaseke na hata Buswita na bila kumsahau Rafael Daud. Beki ya kati kaja Elisha Mroiwa. Sasa tusisajili kwa kulinganisha na wengine angalia dhamira yako ya usajili ni nini. Everton katoka mchezaji lakini hawajasajil kabisa..wakati Man City ameingia Mahrez..Chelsea hadi sasa ni Geoghino. Na mbaya zaidi mwakani hatushiriki mashindano makubwa..tuache nafasi ya dirisha dogo kwa kuangalia mapungufu ya kikosi chetu

      Delete
    2. Sio kweli WACHEZAJI wengi walikumbwa na majeruhi na kwakuwa hakuwepo mastraika mbadala waliokuwa na uwezo wa juu, timu iliishia kupata wakati mgumu, sasa kama malengo ya Yanga ni kushiriki tu

      Delete
    3. Kama malengo ni kushiriki ligi tu, hao wachezaji wanatosha, kuifanya iwanie NAFASI YA sita, au ya sana.lakini kama malengo ni ubingwa, basi Yanga wanajiweka katika nafasi ngumu sana. TUWE WAKWELI HUWEZI KUMTEGEMEA MCHEZAJI MMOJA KATIKA NAFASI YA MSHAMBULIAJI KUNA KUUMIA, NA MATATIZO MBALIMBALI, GAME KUKATAA...LAZIMA UWE NA SUBSTITUTION ZINAZOWEZA KUAMUA MATOKEO, na KUKUPA USHINDI KILA NAFASI INAYOTENGENEZWA....HILI LITAISUMBUA SANA YANGA, LAKINI HALITAKUWA KIKWAZO KWA AZAM NA SIMBA KWANI WAMEFANYA USAJILI KWA KUZINGATIA MAPUNGUFU WALIYONAYO. MASHABIKI WATAPUNGUA VIWANJANI HILI TFF WANATAKIWA KULIFIKIRIA...

      Delete
  6. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic