ALLIANCE YAZIDI KUZIABISHA TIMU ZA LIGI KUU
Timu ya Alliance ya Mwanza imeendeleza ubabe kwa timu za Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jijini Mwanza.
Alliance imezidi kuziaibisha timu ambazo tayari zipo katika ligi kabla yenyewe haijapanda kukipiga msimu ujao kwa kuendeleza kutoa vichapo.
Mbali na kuwachapa Singida, timu hiyo pia iliwafunga Kagera Sugar kwa mabao 2-1 walipokutana katika mchezo uliopita na kuonesha dhahiri shahiri kuwa imejipanga kwa msimu ujao.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbwana Makata, amesema kikosi chake licha ya kushinda bado kina mapungufu kadhaa katika safu ya umaliziaji.
Makata ameeleza atajitahidi kurekebisha makosa hayo kadhaa ambayo anaamini yanaweza kuigharimu timu pale msimu ujao wa ligi utakapoanza Agosti 22.
0 COMMENTS:
Post a Comment