MITAMBO YA KUFA MTU YAANDALIWA KUMUAGA CANNAVARO MOROGORO
Kuelekea mechi ya kumuaga Nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', unaambiwa mitambo ya kufa mtu imeshaandaliwa ndani ya Uwanja wa Jamhuri Morogoro tayari kwa burudani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 tayari kumuaga Cannavaro ambaye ameichezea Yanga kwa mafanikip makubwa.
Yanga itashuka dimbani leo majira ya saa 10 kamili jioni kukipiga na Mawenzi Market inayonolewa na Abdi Kassim 'Babi' ambayo ni maalum kumuaga Cannavaro ambaye ni Meneja wa timu kwa sasa.
Mbali na kumuaga Cannavaro, Yanga itakuwa inatumia mechi hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Agosti 19 2018.
Wasanii mbalimbali watakuwa wanatumbuiza ikiwemo Mr Blue huku wengine kutoka katika tasnia ya filamu ikwemo Wema Sepetu naye atakuwepo.
KWANINI MECHI ISINGEKUWA ILE YA SIMBA NA YANGA NDIYO IWE YA KUMUAGA KANAVARO HUYU MCHEZAJI MUHIMU SANA KWA YANGA ANGESTAHILI MECHI KUBWA YENYE KUJAZA UWANJA WOTE ULIOFURIKA
ReplyDeleteNi sawa mambo mengine tuwaachie viongozi wao ndio wanajua kwanini mawenzi na sio timu nyingine
ReplyDelete