August 3, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuweka kambi ambayo inalekea kufikisha takribani wiki moja huko Kampala, Uganda, uongozi wa Azam umesema kesho kikosi chao kitacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki.

Azam ambao wanafanya mazoezi yao katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Makelele, watakuwa wanacheza na Vipers SC ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini humo.

Kuelekea mechi hiyo, Ofisa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga, amesema lengo na madhumuni ya mechi hiyo litakuwa ni kuwapima na kuwaweka fiti wachezaji kuelekea msimu mpya wa ligi utakaoanza Agosti 22.

Wakati Azam wakitarajia kucheza mechi hiyo, wapinzani wao Simba nao wapo nchini Uturuki ambapo juzi walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mouolodia ya Morocco na kwenda sare ya 1-1 huku mechi ikiisha dakika ya 65 sababu ya mvua kali.

Azam wameamua kuweka kambi nchini humo kutokana na utofauti wa mazingira baina ya Tanzania na Uganda kwa kuwapa wachezaji uhuru na utulivu zaidi tofauti na wakiwa katika jiji la Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinatarajia kurejea nchini mwishoni mwa wiki ijayo tayari kwa maandalizi ya mwisho ya kuanza vipute vya ligi kwa msimu ujao wa 2018/19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic