August 3, 2018


Wakati taarifa zikieleza kuwa klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya kuachana na kipa wake Mcameroon, Youthe Rostand kwa kuvunja naye mkataba, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameibuka na kauli nyingine.

Nyika amefunguka na kueleza kuwa Rostand bado ni mchezaji halali wa Yanga na wala hakuna ukweli juu ya kile kinachoelezwa kuwa ataondoka katika kikosi cha timu hiyo.

Kiongozi huyo amesema watakuwa na la kusema paleviongozo wa Kamati ya Utendaji na Usajili itakapokutana kwa ajili ya kufanya kikao maalum juu ya kikosi kilichoelekea Morogoro.

Nyika ameeleza kamati hiyo itakutana kesho kujadili mambo kadhaa kuhusiana na wachezaji wa Yanga huku ikionekana kuna jambo anaficha japo kwa taarifa za ndani watakuwa wanajadiliana namna ya kumalizana na Rostand.

OMARY KAAYA ANASEMAJE?

Wakati Nyika akiibuka kivingine, Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaaya, naye amesema kuwa hawezi kuzungumzia lolote kuhusiana na kipa Rostand.

Kaaya amesema hawezi kusema kama mchezaji huyo anafaa au hafai kuendelea kuitumikia Yanga kutokana na namna uwezo wake ulivyo.

Kiongozi huyo ameeleza ni vema akatafutwa Jumatatu kwani atakuwa na mambo kadhaa ya kuzungumza ikiwemo sakata la mchezaji huyo.

Hata hivyo uongozi wa Yanga umeitisha kikao na Waandishi wa Habari leo majira ya mchana na jambo ambalo linatarajiwa kuwekwa hadharani ni hatima ya Rostand na klabu hiyo.

3 COMMENTS:

  1. Ni kumuonea tu. Wengi hawajitumi viongozi na wanachama tujitafakari.

    ReplyDelete
  2. Ni kumuonea tu. Wengi hawajitumi viongozi na wanachama tujitafakari.

    ReplyDelete
  3. Rostand ni kipa mzuro sana, tatizo lipo kwa mabeki pale Yanga. Timu haina mabeki makini. Kumlaumu kipa ni kumuonea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic