August 12, 2018


Wakati Simba wakifanikiwa kuuzindua Uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa, Lindi, kuna uwezekano mkubwa wa Yanga pia kuenda kucheza na Namungo siku za usoni.

Kwa mujibu wa Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema kuwa watani wa jadi kwa Simba, Yanga, nao wataenda mkoani humo kwa ajili ya kucheza mechi moja katika Uwanja huo.

Majaliwa ameyasema hayo mara baada ya Simba kukipiga na Namungo ambapo mechi hiyo ilienda suluhu ya kutofungana akisema bado zamu ya Yanga pamoja na Azam FC.

Aisha, Waziri huyo amesema kuwa pia klabu ya Ndanda nayo itawasili Ruangwa kucheza mechi moja kitu ambacho anaamini kitaletea hamasa ya watu wa mji huo kupenda zaidi mchezo wa soka.

Uwezekano wa Yanga kwenda kucheza ndani ya Majaliwa Stadium utafanikiwa baada ya kukipiga na USM Alger ya Algeria Agosti 19 ambapo kikosi chao kipo Morogoro kujiandaa na mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

3 COMMENTS:

  1. WAZIRI ??? HUYU NI WAZIRI MKUU. KWANINI HAMUWI MAKINI NA UANDISHI KWA VIONGOZI WETU WAKUU WA NCHI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAWA WAANDISHI WACHA WAENDELEE KUPIGWA NA POLISI

      Delete
  2. Kuwa makini na uandishi wa habar zako siyo kukurupuka tu,Kasimu Majaliwa ni was wazir mkuu ca kushangaza hakuna hata sehemu moja ambayo umempa hadhi yake
    Mbaya zaidi unamuita Aisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic