August 20, 2018


Na George Mganga

Kwa mdau yoyote ambaye anafuatilia soka la hapa Bongo sidhani kama yupo ambaye hajalisikia jina na Heritier Makambo, mshambuliaji aliyeanza kuonesha cheche Yanga akitokea FC Lupopo ya Congo.

Jina hili limeanza kuwa gumzo kubwa tangu Yanga iweke kambi ya wiki mbili mjini Morogoro ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Wakati Yanga ikiwa Morogoro, Makambo ambaye amekabidhiwa rasmi majukumu ya aliyekuwa mshambuliaji hatari kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma aliye Azam FC kwa sasa, alianza kucheka na nyavu katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Tanzanite Academy huku timu ikishinda mabao 5-1.

Mshambuliaji huyo alikuja tena akatikisa nyavu za Mawenzi Market kwenye mchezo maalum wa kumuaga aliyekuwa beki wa timu hiyo, mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa kupachika bao moja na la ushindi, mechi Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Jana tena Makambo amezidi kuwakonga mioyo mashabiki na wadau wa klabu ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi dhidi ya USM Alger, mchezo ukiwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Baada ya kuonesha utulivu na umakini wa kutosha kutokana na namna alivyosakata kambumbu Uwanjani, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameibuka na kuanza kumlinganisha mchezaji huyo na straika hatari wa Simba, Emmanuel Okwi.

Jeuri hiyo imetokana na uwezo ambao ameonesha Makambo kwa kutupia bao la pili mnamo dakika ya 46 ikiwa ni baada ya kiungo mshambuliaji Deus Kaseka kuandika la kwanza dakika ya 42 ya kipindi cha pili.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamesema ni mapema sana kuanza kumfananisha Makambo na Okwi kutokana na uchache wa mechi ambazo wamecheza pamoja na makubwa ambayo Okwi ameyafanya hapa nchini tangu aanze kuichezea Simba.

Aidha, mashabiki hao baadhi wameanza kuwazodoa watani zao wa jadi wakiamini Makambo atawapa wakati mgumu pindi watakapokutana na Simba na hata timu nyingine zinashiriki ligi na hii imechagizwa pia na urejea wa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

Manji alirejea kwa mara ya kwanza tangu atangaze kuachia ngazi kuwashuhudia Yanga wakikipiga na USM Alger na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufikisha alama 4 kwenye kund D.

Baada ya kumalizana na USM, Yanga sasa inaelekeza nguvu zake kukamilisha mechi za kundi hilo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, mchezo utakaopigwa huko Kigali, Rwanda Agosti 28 2018.

6 COMMENTS:

  1. Bado sana kumfikia Okwi huyo makambo wenu

    ReplyDelete
  2. Acheni kufananisha okwi na vitu vya jabu

    ReplyDelete
  3. Kwani Okwi mungu mpaka asifananishwe na binadamu mwingine

    ReplyDelete
  4. Hana lolote huyo okwi kumpa sifa tu bure mbn juzi hakufunga?

    ReplyDelete
  5. Kwaniokwi ananini cha kutisha ndio mahana mnava jezi za waganga

    ReplyDelete
  6. Kwaniokwi ananini cha kutisha ndio mahana mnava jezi za waganga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic