August 29, 2018


Baada ya awali taarifa kusambaa kuwa klabu za Simba na Lipuli zimekubaliana kuliandikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) barua ya kuliomba wacheze mechi yao ya ligi kama ambavyo ilikuwa imepangwa, uongozi wa Lipuli umekuja na kauli tofauti.

Lipuli wameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa ya kuahirishwa kwa mechi yao na Simba ambayo ilipaswa kupigwa Septemba Mosi 2018 waliamua kurejea kwao Iringa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo baada ya Simba.

Juzi Shirikisho la Soka Tanzania kupitia kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, alisema wameamua kuahirisha mechi zinazohusisha timu za Simba, Yanga na Azam kutokana na wachezaji wake kuitwa timu ya Taifa Stars.

Mapema baada ya Lipuli kupata taarifa hizo wakati wakiwa Dar es Salaam waliamua kuondoka kurejea Iringa na mpaka muda huu wapo mjini humo.

Aidha, mbali na kuondoka, Lipuli wamesema watazungumza na TFF kuona namna gani wanaweza kufidia gharama zao ambazo walizitumia wakati wakiwa Dar es Salaam kutokana na kuweka kambi pamoja na chakula.

Mabosi wa timu hiyo wameeleza hayo kutokana na timu yao kuwa na hali ngumu ya kifedha jambo ambalo limekuwa likizisumbua timu nyingi ndogo kutokana na kukosa wafadhili.

Wachezaji wa Simba, Yanga na Azam waliitwa kwa ajili ya kuja kujiandaa na mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON ambapo wataingia kambini Agosti 30 tayari kujiandaa na mechi hiyo itakayopigwa Septemba 8 dhidi ya Uganda huko Kampala.


1 COMMENTS:

  1. Kwani Kanuni za TFF zinasemaje? timu ngeni inatakiwa kusafiri kufika kwenye mchezo na timu wenyeji siku ngapi kabla ya mchezo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic