August 29, 2018


Baada ya kuanza kwa kuboronga katika mechi za ufunguzi wa Ligi Kuu Bara, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewasimamisha waamuzi 6 kuchezesha mechi mpaka pale Kamati ya Saa 72 itakapopitia masuala kadhaa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Umande Chama, amesema kuwa wameifika hatua ya kufanya vivyo kutokana na kuliangusha shirikisho la ligi kwa ujumla.

Chama amesema waamuzi waliosimamishwa wengi ni wale wa pembeni, au washika vibendera baada ya kushindwa kumudu kuchezesha mechi vizuri na kupelekea malalamiko kwa timu husika.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa mechi kadhaa ikiwemo ile ya Yanga dhidi ya Mtibwa, Azam FC dhidi ya Ndanda FC zimekuwa na mapungufu ambayo yanapswa kuwaadhibu waamuzi waliochezesha.

Kutokana na mampungufu hayo kujitokeza, TFF imeamua kuwasimamisha kwa muda waamuzi wote sita ili kuipa nafasi Kamati ya Masaa 72 kufanya uchunguzi kisha kujadiliana na kuja na mwafaka wa hukumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic