August 2, 2018


Imeripotiwa kuwa beki wa kimataifa wa Uganda, Juuko Murushid amerejea katika klabu ya Simba baada ya mipango ya kujiunga na SuperSport United FC kushindwa kufanikiwa.

Mchezaji huyo aliondoka nchini baada ya msimu wa ligi 2017/18 kumalizika na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kukamilisha dili hilo ingawa taarifa zinaeleza kuwa limefeli.

Murushid sasa ataendelea kusalia Dar es Salaam kukisubiria kikosi cha Simba ambacho kipo nchini Uturuki kujiandaa na tamasha la Simba DAY pamoja na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe beki huyo bado amebakiza mwaka mmoja hivyo kuna nafasi kubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi katika msimu ujao.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuanza kurejea nchini Agosti 5 2018 kwa ajili ya tamasha lake ambapo kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana tarehe 8 Agosti.

7 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Dirisha la usajiri mbona lilikwisha fungwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. "Ikumbukwe beki huyo bado amebakiza mwaka mmoja hivyo kuna nafasi kubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi katika msimu ujao".Nimenukuu

      Delete
  3. Dirisha limekwisha fungwa na mbona simba awakumjumuisha kwenye usaji waliopeleka tff

    ReplyDelete
  4. Dirisha la wachezaji wa kigeni kama niko sahihi linafungwa 6th August

    ReplyDelete
  5. Safi sana. Simba na viongozi wake naweza kusema wanaweza kutulia sasa kwani timu inaonekana kukamilika kila idara. Ninachokiomba kwa moyo wa dhati kabisa kwa mapenzi na mafanikio ya klabu pendwa ya Simba wanatakiwa kukaa chini na Juuko na kuzungumza nae kwa undani kabisa ili kumuweka sawa kiakili na kimwili. Juuko anaweza kukosa kambi ya Uturuki lakini kitendo cha viongozi wake wa Simba kukaa nae kujua kama kuna kitu chochote kinamtatiza ni kitu muhimu na ni moja ya pre season iliobora kabisa watakayompa Juuko. Siwezi kumtia wawa kwenye thamani juu ya Juuko hata siku moja. Juuko kiumri bado mchanga mbele ya wawa. Juuko hana history ya major injury kwa kiasi fulani unaweza kusema yuko fit kimwili ila kiakili inaonekana kuna kitu hakimrizishi pale Simba sasa ni wakati kwa viongozi wa Simba kuzungumza nae kwani ni moja kati ya mabeki kazi kweli kweli anapokuwa sawa.

    ReplyDelete
  6. Wote ni wachezaji WA simba tuwapatie nafasi sawa kwa kuitumikia simba yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic