YANGA SHUGHULI IMEWASHINDA WAJIPANGE KWENYE LIGI TU
Na Seleman Matola
Bado siku 22 kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani ambao utapigwa Agosti 18, mwaka huu mkoani Mwanza.
Safari hii mchezo huo utazikutanisha timu ya Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa wa Kombe FA dhidi ya Simba ambao ni mabingwa wa msimu uliopita wa Ligi kuu Bara.
Baada ya mchezo huo ligi kuu itakuwa imefunguliwa rasmi ambayo kwa msimu huu itakuwa na ongezeko la timu nne na kufikia 20 kutoka 16 za msimu uliopita huku zikishuka timu mbili kutoka ligi kuu kwenda daraja la kwanza.
Naamini ligi ya msimu huu inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki mbalimbali na wengi wakitaka kuona wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye timu wakiwasha moto licha ya kwamba msimu huu kutakuwa na idadi kubwa ya makocha wa kigeni kwenye ligi yetu.
Lakini siyo makocha pekee ambao wameongezeka hadi idadi ya wachezaji wa kigeni imeongezwa kutoka wachezaji saba wa msimu uliopita hadi kufikia 10 ambao inaelezwa wachezaji hao wanaweza kucheza wote katika mechi moja.
Niwapongeze Shirikisho la Tanzania (TFF) kwa kuanza kutekeleza maagizo ya serikali yetu kwa kuamua kuanza kumuita mshambuliaji wa Leicester City ya England, Mtanzania, Ben Anthony Starkie ambaye alitua nchini wikiendi iliopita.
Mshambuliaji huyo ambaye anacheza katika timu ya vijana U-16, ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana U17, maarufu kama Serengeti Boys kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika (Afcon) kwa vijana Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘Cecafa Zone’.
Kinda huyo ameitwa kwenye kikosi hicho kutokana na TFF k u t e k e l e z a maagizo ya Mk u r u g e n z i wa Wizara ya Habari Sanaa U t ama d u n i na Michezo, Yusuph Singo ambaye aliiagiza kuanza kusaka vipaji vya Watanzania wanaocheza soka nje ili kuzisaidia timu za taifa.
M a a g i z o hayo yalikuja baada ya kushuhudia mchezaji mwenye asili ya Kitanzania, Yussuf Yurary Poulsen, aliyechezea kwa mafanikio akiwa na taifa ya Denmark katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika hivi karibuni nchini Urusi.
Hoja yangu kwa siku ya leo, nataka kuwekana sawa juu ya wawakilishi wetu wa mi c h u a n o ya kimataifa ambayo bado wana ende l e a nayo hadi sasa, hapa n a w a z u n gumzia Yanga ambao wanashiriki Kombe la S h i r i k i s h o Afrika.
Yanga wan a s h i r i k i katika michuano na w i k i e n d i iliyopita walicheza mechi yao ya nne dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambao walipoteza kwa kipigo cha mabao 3-2 na katika mechi ya kwanza walifungwa na Wakenya hao mabao 4-0.
Katika michuano hii Yanga wapo kundi D wakishika mkia na pointi yao moja, Gor Mahia anashika nafasi ya kwanza akiwa na pointi nane sawa na USM Alger wanashika nafasi ya pili wakati Rayon Sport wakiwa wanashika nafasi ya tatu. Ni wazi kabisa kwamba Yanga na Rayon wameshatoka na kilichobaki ni kukamilisha ratiba kwa mechi mbili zilizobaki.
Lakini kilichopoteza kwanza wingi wa majeruhi na ukata wa kiuchumi ambao unatesa ila ninachotaka kuwaeleza waanze kujiandaa na ligi katika wakati huu kwa kuwa huko katika kombe la Shirikisho wametolewa ili kuleta ushindani kweli kwenye ligi yetu sawa na timu nyengine.
0 COMMENTS:
Post a Comment