August 31, 2018


Na George Mganga

Kocha wa timu ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amekutana na wachezaji Simba aliowaondoa kwenye kikosi chake baada ya kuchelewa kuripoti kambini.

Baada ya kukutana nao, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo ametoa taarifa kuwa suala hilo limekwisha na kwamba hakuna kitakachozuia nyota hao kuitwa tena Stars kama tu wataonyesha kiwango kizuri kwenye klabu yao.

Ndimbo ameeleza kuwa Amunike ameshamalizana na wachezaji wa Simba na atawaita tena endapo wataonesha kiwango kizuri ambacho kitamshawishi wakiwa kwenye klabu yao.

Licha ya kusamehewa, wachezaji hao wataukosa mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda, Septemba 8 2018 huko Kampala.

Nyota hao sita watakosekana kutokana na nafasi zao kujazwa na wachezaji wengine ambao tayari wameshaanza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.

13 COMMENTS:

  1. HAINA MAANA KAMA HAWACHEZI NA UGANDA

    ReplyDelete
  2. Nijambo la busara kubwa sana ambalo lilihitajika tokea mwanzo. Sasa tuna imani kubwa na kocha na tunamuombea kila la heri, lakini pia wachezaji hao wenye mazowea na uwezo makubwa katika mechi za mataifa haraka waunganishwe kwasababu hawajachelewa hsta kidogo si kitu kuwa badili yao wameshachaguliwa lakini kwa papara na wengi wao hawana ujuzi wa mataifa na badae watachaguliwa walio bora na hapo ndipo maana ya kusamehewa. Tunakushukuru kocha na wote waliofanikisha hayo na yalihitajika toka mwanzo kuepukana na lawama na malalamiko kila kila kona

    ReplyDelete
  3. Yes, the weak can never forgive. Forgiveness is the attribute of the strong

    ReplyDelete
    Replies
    1. YOU FORGIVE FOR WHAT? AND WHAT DOES THAT FORGIVENESS MEAN WHEN THE PLAYERS WILL NOT PLAY IN THE COMING MATCH AGAINST UGANDA WHICH IS A CRUCIAL MATCH? WHY DIDNT THE COACH MEET WITH THE PLAYERS BEFORE HE SLAMMED THE BAN? WRONG DECISION FUELLED BY EMOTIONS.

      Delete
  4. Ujinga kabisa. Waafrica wazuri wa kutengeneza majungu hakuna jengine. Tayari Taifa Stars imesha gawanyika kabla hata ya kuingia uwanjani. Watanzania ni watu wa amani na mshikamano na siku zote huo ndio msingi wa maisha yetu hata makazini. Kocha wa Stars na TFF wanalengo ya kuwanganya watanzania kitu amabacho ni hatari. Hakika kama mechi hii ya Uganda ingekuwa inachezwa Dar pale Taifa basi watu wa Simba wangesusia mechi hiyo. Busara ni ishara ya ukomavu wa mtu kiakili.

    ReplyDelete
  5. Kusamehe kwa kosa lipi?Kanuni inasema wachezaji wanapaswa kuripoti siku 3 kabla kwa mujibu wa FIFA.Ukiwataka kabla ni lazima uombe kwa klabu sy kuwe na mashindano ya mfululizo kama Kombe la dunia au fainali za mataifa za CAF.Vingivevyo ni ubabe tu usiokuwa nä faida yeyote.Kama wamekosea tuelezwe wamevunja kanuni ipi?

    ReplyDelete
  6. Subirini kwanza Taifa Stars ifungwe na Uganda Cranes..Tutimize lengo..
    Tukishafungwa baadaye tutawaita tu!

    ReplyDelete
  7. Wamemuaibisha Amonika. Sote tulifahamu kuwa ni yeye aliyewafukuza wachezaji na tukajiuliza huyu kovha mpya
    kazipata wapi nguvu za kufukuza baada ya kufika tu, kumbe si yeye na walitaka kumharibia ili wafurahi

    ReplyDelete
  8. Matatizo yetu makubwa Watanzania ni kujisahau, kusahau na kutojitambua. Hatujui tunataka nini na kwa wakati gani. Kujengwa nidhamu katika masuala yanayotuhusu linaonekana ni jambo la kiadui!!! Tunataka soka au mafanikio bila kupata uchungu wake. Tunaitaka pepo bila kuitafuta hii ni miujiza.
    Wengi wetu hatuna weledi lakini matamanio yetu yanatupelekea kuwakosoa wenye weledi. Inasikitisha sana.
    Timu yetu ya Taifa pamoja na hao walioachwa kuwemo haijapata kupata mafanikio yenye tija sasa kwanini wengine wasijaribu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. TUWACHUKUE WACHEZAJI WA TIMU ZA DIVISION 4 NDIO WAKACHEZE NA UGANDA CRANES ?

      Delete
  9. HUU NI UTOTO WATU WAZIMA HUFANYA MAAMUZI MAKUBWA BAADA YA KUTAFAKARI FAIDA NA HASARA YA KUAMUA JAMBO HASA KAMA NI SUALA LA WATU WENGI. KOCHA ANAAMUA KUFUKUZA WACHEZAJI 7 LEO BAADA YA SIKU 3 NA BAADA YA WATU KUONYESHA HISIA ZAO ZA KUTORIDHIKA NA MAAMUZI HAYO, KOCHA HUYOHUYO ANAWASAMEHE WACHEZAJI LAKINI WASICHEZE MECHI NA UGANDA. KATIKA KUNDI LETU, TIMU NGUMU NI UGANDA. SASA MSAMAHA HUU UMEISAIDIA NINI NCHI YETU? AIBU. TOKA MWANZO KOCHA ALIKURUPUKA KUAMUA KUTIMUA WACHEZAJI BILA KUJUA SABABU. TFF ILIMJAZA USHAURI MBAYA. KATIBU MKUU TFF ANASIMULIA ALIVYOWAPIGIA SIMU USIKU SAA SABA WACHEZAJI KUWAAMBIA FAIDA YA KUCHEZEA TIMU YA TAIFA, AMA KWELI TFF INA UTARATIBU HUO WA KIOFISI? BARUA ZIKO WAPI KWA WACHEZAJI? UTAMLAUMU MTU KWA SIMU YAKE KUTOPATIKANA SAA SABA USIKU? AIBU SANA. UGANDA WAKITUFUNGA NI KWASABABU TAYARI TUMEJICHANGANYA WENYEWE HATUNA SABABU YA KUFUNGWA NA UGANDA TUNA WACHEZAJI WAZURI NI KOCHA TU ANAKOSEKANA WA KUUNGANISHA TIMU. SASA HUYU KOCHA ANAANZA KWA KUINGIA KWENYE MGOGORO USIO NA TIJA NA NI TFF WANASABABISHA YOTE HAYA

    ReplyDelete
  10. COACH AMUNIKE MADE A WRONG DECISION. HE HAS BEEN UNFAIR TO THE SIMBA PLAYERS WHO HAVE BEEN DROPPED FROM THEIR OWN NATIONAL TEAM. HONESTLY YOU CAN NOT BE RESPECTED IF YOU CANT SHOW RESPECT TO OTHER PEOPLE INCLUDING THE PLAYERS. I AM SO SAD THAT WE ARE GOING TO SEE UNHAPPINESS AMONG OUR FOOTBALL FANS WHEN WE PLAY UGANDA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic