August 27, 2018


Meneja wa Arsenal Unai Emery anatarajia mchango zaidi kutoka kwa kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 29, aliyekosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Westham kutokana na kuugua. Arsenal walishinda 3-1. (Mirror)

Beki wa Brazil David Luiz, 31, anasema huenda angelazimika kuihama Chelsea iwapo Antonio Conte angesalia kama meneja wa klabu hiyo. (Sky Sports)

Mlindalango wa Liverpool Simon Mignolet, 30, anasema inashangaza kwamba klabu hiyo ya Anfield ilimruhusu kipaLoris Karius kujiunga na Besiktas ya Uturuki kwa mkopo. Mbelgiji huyo anasema hajui mustakabali wake katika klabu hiyo ya England. (Liverpool Echo)

Beki wa Tottenham Danny Rose, 28, huenda akahamia Marseille - kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu - katika juhudi zake za kutaka kujiimarishia nafasi ya kucheza katika timu ya taifa ya England. (Star)

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amewaambia wachezaji wake kwamba wote ni lazima wamridhishe tena baada yake kulazimika kuwatumia wachezaji mbadala kutokana na baadhi yao kushiriki Kombe la Dunia. (Telegraph)


Meneja wa Newcastle Rafael Benitez amesema anaridhishwa na uamuzi wa kuchelewesha mazungumzo kuhusu mkataba wake mpya hadi mwaka ujao. Mhispania huto alitarajiwa kutia saini mkataba mpya kabla ya msimu lakini sasa anasema anafikiria tu kuhusu mechi. (Goal)

Benitez alimwacha nje nahodha wa klabu hiyo ambaye pia ni beki Jamaal Lascelles kutoka kwa mechi ya Jumapili ambayo walishindwa 2-1 na Chelsea baada yao kuzozana mazoezini kuhusu mbinu za kutumiwa kwenye mechi hiyo. (Mail)


Mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 32, alikataa ofa ya kujiunga na Manchester United. (Calciomercato kupitia Sun)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic