August 13, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana ameanza rasmi mpango wa kuviwezesha kiuchumi vilabu vya Jogging kwa kuvipatia mitaji ya kuwezesha kuanzisha miradi ya kujikwamua kiuchumi.

Aidha amesema anachokitaka kwa sasa ni kuona vilabu vya Jogging vinashiriki shughuli za uzalishaji Mali ili wajikwamue kiuchumi na wasipate muda wa kushiriki matukio ya uhalifu kama uporaji, ubakaji na matumizi ya dawa za kulevya.

Makonda amesema kila baada ya miezi miwili yatakuwa yakifanyika mabonanza makubwa ya Jogging hivyo amezitaka kila wilaya kujiandaa.

Pamoja na hayo amewataka vijana mkoani kwake kuchangamkia fursa zote halali zinazopatikana Dar es salaam kwakuwa mkoa huo Ndio chimbuko la mafanikio kwa wengi huku akiwahimiza kumtanguliza Mungu kwa kila jambo.

Hata hivyo mkuu huyo amewaomba Vijana wa Jogging kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu ili Dar es salaam iendelee kubaki kuwa jiji lenye amani na usalama wakati wote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic