MASAU ASEMA ALITAMANI KUANZA NA SIMBA LIGI KUU, ADAI WAMEIKWEPA RUVU
Kuelekea msimu wa Ligi Kuu Bara unaotaraji kuanza Agosti 22, Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa alitamani kama ratiba yao ingeanza na Simba.
Tambo za Bwire zimeanza kutokana na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa awali kwenye msimu uliopita kwa jumla ya mabao 7-0.
Msemaji huyo amefunguka na kusema kuwa itakuwa Simba waliomba ratiba ibadilishwe ili wasianze na Ruvu Shooting kwa hofu ya kuogopa kipigo.
Licha ya kupiga kambi ya wiki mbili Uturuki, Bwire amesema Simba hawana lolote jipya hivyo watawanyoosha pale watakapokutana awamu hii.
Bwire ameeleza vilevile kikosi chao kipo mawindoni hivi sasa kujiandaa na mechi za simu ujao huku akisema watakuwa hawashikiki.
Kila mwaka tusubiri msimu ujao. Ngoja ugongwe kumi bila safari hii ushike adabu
ReplyDeleteHuyu masau Bwire ana matatizo gani huyu kila mwaka anagongwa lakini haichi mdomo subiri kuna Siku atakula goli kumi ndio akome
ReplyDeleteH
ReplyDelete