MASIKINI OMMY DIMPOZ, HALI YAKE SI NZURI, APELEKWA TENA AFRIKA KUSINI
Staa wa Bongo Fleva, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amerudishwa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwa ajili ya matibabu baada ya hali yake kuendelea kutokuwa vizuri licha kutolewa hospitalini huko siku chache zilizopita.
Dimpoz ambaye miezi miwili iliyopita alifanyiwa upasuaji mkubwa wa koo nchini Afrika Kusini, hali yake imekua haiimariki ipasavyo jambo lililosababisha kupandishwa ndege na kurudishwa tena huko kendelea na matibabu zaidi.
Kabla ya kurudishwa Sauzi, katika video aliyoiweka mtandaoni juzi na kuitoa baada ya muda mfupi, ilimwonyesha Dimpoz akiwatakia Waislam wote, Sikukuu njema ya Idd El Haji na kusema kwa sasa hali yake anaendelea ku-recover.
Imeelezwa kwamba, Gavana wa Mombasa nchini Kenya, Hassan Joho ndiye amekuwa msitari wa mbele kumsaidia Dimpoz katika matibabu yake baada ya kumgundua kuwa ana tatizo katika koo lake alipomwona akipata shida kumeza chakula kwenye harusi ya msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Alikiba iliyofanyika Mombasa miezi michache iliyopita.
Joho alichukua jukumu la kumpeleka Dimpoz kwa daktari wake na baada kufanyiwa vipimo vya awali na kugundua tatizo hilo, alipelekwa Sauzi kufanyiwa vipimo zaidi, matibabu na upasuaji ambako amekaa kwa miezi miwili kabla ya kurejea tena Mombasa.
Hata hivyo Watanzania na mashabiki wake walioguswa na tatizo hilo, wamekuwa wakijitoa kuchangia chochote na kumuombea msanii huyo apone ili arejee kujiunga nasi ktk ujenzi wa Taifa letu Tanzania.
“Global Publishers tunakuombea Ommy Dimpoz Mwenyezi Mungu, akuondolee maumivu, akujalie upone haraka, Watanzania na mashabiki zako duniani kote tunatamani kukuona tena ukiwa jukwaani ukiendeleza kile ambacho Mungu amekujalia, tunakuombea kaka, tuna imani kubwa utapona haraka.”
Kutoka Global Publishers
0 COMMENTS:
Post a Comment